Pata taarifa kuu
NIGER-MAREKANI-MALI-USALAMA

Niger yakubali Marekani kutumia ndege zisizo na rubani katika ardhi yake

Serikali ya Niger, imekubali kutumiwa kwa ndege za kivita zisizokuwa na rubani kutumika kuyashambulia makundi ya kigaidi katika mpaka wa nchi hiyo na Mali.

Askari wa Niger wakipiga doria katika jimbo la Ayorou, kaskazini magharibi mwa Niamey, Niger (picha ya zamani).
Askari wa Niger wakipiga doria katika jimbo la Ayorou, kaskazini magharibi mwa Niamey, Niger (picha ya zamani). © ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya magaidi kuwauwa wanajeshi wanne wa Marekani, baada ya kuwashambuliwa wakipiga doria mwezi Oktoba nchini Niger.

Mbali na kusaidia katika vita dhidi ya ugaidi, Marekani imetuma wanajeshi wake karibu 800 kuendelea kufanya mazoezi ya kupambana na ugaidi nchini Niger.

Kundi la Boko Haramu limekua likiendesha vitendo vyake viovu katika nchi za Niger, Nigeria, Mali, Chad na Cameroon.

Maelfu ya watu wameuawa katika mashambulizi ya Boko Haram na wengi wanaendelea kushikiliwa mateka na kundi hilo, huku wengi wakiyahama makazi yao kwa kuhofia usalama wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.