Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Watu 50 wauawa katika uvamizi wa kikabila nchini Sudan Kusini

Watu 50 wameuawa katika mapigano ya kikabila Mashariki mwa nchi ya Sudan Kusini. Haya ni mapigano ya hivi karibuni ya kikabila katika nchi hiyo inayoendelea kukabiliwa na mapigo ya mara kwa mara tangu mwaka 2013.

Wanajeshi wa Sudan Kusini
Wanajeshi wa Sudan Kusini REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya ndani Dut Achuek, amethibitishia kutoka kwa mauaji hayo katika jimbo la Jonglei.

Watu waliouawa ni wanawake 23 na wanaume 19. Mbali na mauaji hayo, makaazi yao yaliteketezwa moto.

Kabila la Murle lilivamia kabila la Dinka katika vijiji wanavyoishi na kuanza kuwashambulia kabla ya kuwaangamiza.

Makabila hayo mawili yanayojishughulisha na ufugaji, yamekuwa yakipigana kwa muda mrefu kutokana na mzozo wa wizi wa mifugo.

Mauaji mabya yalitokea mwaka 2012 kati ya makabila ya Nuer na Murle na kusababisha vifo vya watu 3,000.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.