Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-UCHAGUZI-SIASA

Rais mtarajiwa wa Zimbabwe awataka raia wake kudumisha demokrasia

Kiongozi mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, ambaye alirejea nchini jana Jumatano jioni baada ya kukimbilia uhamishoni akihofiwa kuuawa amewataka wananchi wa Zimbabwe kudumisha amani na demokrasia.

Makamu wa rais wa zamani wa Zimbabwe na kiongozi mpya wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa aliwahutubia wananchi mjini Harare baada ya kurudi kwake kutoka uhamishoni Novemba 22, 2017.
Makamu wa rais wa zamani wa Zimbabwe na kiongozi mpya wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa aliwahutubia wananchi mjini Harare baada ya kurudi kwake kutoka uhamishoni Novemba 22, 2017. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo hali ya usalama nchini Zmbabwe imeimarishwa baada ya kuwasili kwa Emmerson Mnangagwa.

Watu waliokua wakimsubiri mchana kutwa kwenye uwanja wa ndege wa Harare walirudishwa na nyuma na vikosi vya usalama na ulinzi, huku wakitakiwa kujielekeza kwenye makao makuu ya chama tawala cha Zanu-PF.

Baada ya siku nzima ya kusubiri, Emmerson Mnangagwa alifanya kurudi kwa busara. Ilikuwa mwisho wa siku ambayo alionekana kwa umma. Wafuasi wake walimngojea kwenye uwanja wa ndege siku ya Jumatano mchana, lakini jeshi hilo liliwafukuza, wakiwaomba kurudi katikati ya jiji, kwa makao makuu ya chama tawala, Zanu-PF.

Bw. Mnangagwa aliwasili baada ya masaa machache, akizungumza na umati uliozungukwa na askari kadhaa wa kikosi cha ulizi wa taifa, baadhi wakiwa mbele yake, ishara ya hali ya wasiwasi inayoendelea kuhusu usalama wake. Makamu wa rais wa zamani alitoroka nchi yake wiki tatau zilizopita baada ya kufutwa kazi na Robert Mugabe, akisema akuhofia kuuawa.

Katika hotuba yake, iliyokolezwa na maneno yaliyokuwa yakitumika wakati wa vita vya uhuru wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa alilishukuru jeshi la nchi hiyo, ambalo liliingilia kati baada ya yeye kufukuzwa na Rais Robert Mugabe na kuweza kufanikisha hali iliyopo sasa kwa amani.

Mnangagwa, ambaye anatarajia kuapishwa kushika wadhfa wa urais wa nchi hiyo siku ya Ijumaa, amesema kipaumbele chake ni kujenga upya uchumi wa nchi hiyo na kuunda ajira mpya kwa idadi kubwa ya watu wasio na ajira

Katika umati wa watu, hasa vijana wengi, wanachama wa Zanu-PF, wanaona katika utawala wa Mnangagwa kutakua na mabadiliko mengi. "Tumpe nafasi. Tunatarajia kuwa ataleta mabadiliko makubwa, na kama haitakua hivo, hatutakua na budi ya kumuondoa madarakani, kama tulivyomfanya Robert Mugabe, mmoja wa vijana hao amesema."

"Nadhani tunapaswa kumsaidia 100%," amesema mtu mmoja. Huyu ndiye mtu atakae kabiliana na hali inayojiri Zimbabwe. Amekuwa katika siasa kwa muda mrefu, ana uhusiano mzuri na kila mtu. Kwa namna fulani, yeye anaona mbali kwa njia yake mwenyewe. "

Kwa upande wa chama kikuu cha upinzani cha MDC, wanasema serikali ya mpito ambayo inanapaswa kujikita na maandalizi ya uchaguzi kuanzia mwezi Julai mwaka ujao, kama ianavyoelezwa na Katiba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.