Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-USALAMA

Jeshi lakanusha kuepo kwa mapinduzi ya kijeshi Zimbabwe

Jeshi la zimbabwe limekanusha kuepo kwa mapinduzi ya kijeshi. Mapema asubuhi jeshi la Zimbabwe limedhibiti kituo cha habari cha taifa ZBC.

Askari akisoma taarifa kwenye televisheni ya kitaifa ya ZBC, usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano, Novemba 15, 2017. Jeshi lilidai kuwa limeingilia kati dhidi ya "wahalifu" walio karibu na Rais Mugabe.
Askari akisoma taarifa kwenye televisheni ya kitaifa ya ZBC, usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano, Novemba 15, 2017. Jeshi lilidai kuwa limeingilia kati dhidi ya "wahalifu" walio karibu na Rais Mugabe. capture d'écran ZBC
Matangazo ya kibiashara

Mapema Jumatano asubuhi Novemba 15 kwenye televisheni ya taifa, maafisa wa juu katika jeshi la nchi hiyo wamekanusha kuepo kwa mapinduzi ya kieshi.

Hali hii ilianza mapema alfajiri. Mashahidi wanasema milipuko kadhaa ilisikika katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, na askari wamedhibiti kituo cha habari cha taifa ZBC. Hali ya sintofahamu inaendelea nchini humo.

Saa 10:00 afajiri,katika tangazo lililorushwa kwenye televisheni ya taifa, jeshi lilikanusha kuepo kwa mapinduzi ya kijeshi nchini Zimbabwe. Sio "mapinduzi ya kijeshi", jeshi lilithibitisha.

Jeshi lilisema kwamba Robert Mugabe na familia yake wako salama. Muda mfupi kabla, shirika la habari la AFP, likimnukuu shahidi mmoja, lilisema kuwa milio ya risasi ilisikika karibu na makazi binafsi ya rais Mugabe. "Tunalenga wahalifu walio karibu naye ... wakati lengo letu litakamilika, tunatarajia kurejea kwa hali ya kawaida," afisa mmoja wa ngazi ya juu katika jeshi alisema.

Ubalozi wa Marekani wawataka wananchi wa Marekani kusalia makwao

Katika taarifa yake, balozi wa Marekani mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini, amewataka wananchi wa Marekani wanaoishi nchini Zimbabwe kusalia makwao. Pia alirusha ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter akisema "Kutokana na hali tete nchini Zimbabwe, wafanyakazi wa Ubalozi wa Marekani mjini Harare watapunguzwa na kufungwa kwa umma Novemba 15. Wafanyakazi wa Ubalozi wataendelea kufuatilia kwa karibu hali inayoendelea nchini Zimbabwe. "

Pia ubalozi wa Uingereza umewataka raia wa nchi hiyo waishio Zimbabwe kusalia makwao.

Ubalozi wa Canada umetangaza kufungwa kwa ofisi zake baada ya hotuba ya kijeshi.

Onyo la Mkuu wa Jeshi

Kamanda mkuu wa jeshi la Zimbabwe alionya kuingilia kati iwapo pande pinzani zitaendelea kuzozana ndani ya chama tawala cha Zanu-PF.

Katika taarifa isio ya kawaida , Jenerali Constantino Chiwenga alitaka kusitishwa kwa vita dhidi ya wanachama waliopigania uhuru wa taifa hilo.

Matamshi yake yanajiri baada ya rais Robert Mugabe kumfuta kazi makamu wake wa rais aliyetarajiwa kumrithi Emmerson Mnangagwa.

Hali hii inatokea tokea katika mazingira ya mvutano mkubwa. siku ya Jumanne, mizinga ya jeshi iliripotiwa karibu na mji mkuu wa Zimbabwe, na kuchochea uvumi wa mapinduzi ya kijeshi. Uvumi ambao ulikanushwa, ikiwa ni pamoja na Zanu-PF, chama cha rais Mugabe, kwenye Twitter.

Uvumi huu pia ulikanushwa na balozi wa Zimbabwe nchini Afrika Kusini, ambaye alihakikisha kuwa serikali ya Rais Mugabe iko "salama".

Vijana wasema Jenerali wa jeshi hana nguvu zozote Zimbabwe

Siku ya Jumanne Novemba 14, vugu vugu la vijana wa chama tawala cha Zimbabwe lilimkosoa jenerali wa jeshi mwenye cheo cha juu zaidi nchini humo kufuatia kauli aliyoitoa kwamba jeshi linajiandaa kuingilia kati kumaliza mzozo wa ndani wa chama tawala cha Zanu-Pf..

Vugu vugu hilo liliambia vyombo vya habari mjini Harare kwamba mkuu huyo wa jeshi haungwi mkono na jeshi lote.

Wiki iliyopita, Rais Robert Mugabe alimfuta kazi Makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa, na nafasi yake ilikua inatarajiwa kuchukuliwa na mkewe, Grace Mugabe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.