Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-UCHAGUZI-SIASA

Aliyekuwa makamu wa rais wa Zimbabwe atoroka

Makamu wa rais wa Zimbabwe aliyefutwa kazi Emmerson Mnangagwa amelazimika kuimbia nchi yake kufuatia vitisho vya kuuawa, kwa mujibu wa washirika wake wa karibu, siku chache baada ya kutimuliwa mamlakani.

Aliyekua makamu wa rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, almaarufu "Mamba" amekua ni adui wa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na mkewe Grace Mugabe.akawa Rais wa Zimbabwe juu ya Jumatano, Desemba 10.
Aliyekua makamu wa rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, almaarufu "Mamba" amekua ni adui wa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na mkewe Grace Mugabe.akawa Rais wa Zimbabwe juu ya Jumatano, Desemba 10. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Mkewe Rais Robert Mugabe, Grace Mugabe amekuwa akipigania kung'atuliwa kwa makamu huyo katika mkutano maalum wa chama tawala cha Zanu-PF mwezi Ujao.

Hivi karibu Bi Mugabe alimshtumu Emmarson Mnangagwa kwamba alikua akipanga njama za kumpindua mumewe.

Naye Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 93, amemshtumu aliyekuwa makamu wake kwa kupanga njama za kuchukua mamlaka kutoka kwake.

Rais Robert Mugabe alimtaja Bw. Mnangagwa kuwa miongoni mwa waliopanga njama na akaonya kuwa atawachukulia hatua maafisa wengine wa chama hicho walioshirikiana na makamu wake wa zamani.

Wakati huo huo chama tawala cha Zanu PF kilimfuta Mnangagwa katika chama hicho siku ya Jumatano.

Nafasi ya Emmerson Mnangagwa inatazamiwa kuchukuliwa na mkewe robert Mugabe, Grace Mugabe, na hivyo kuwa na urahisi wa kumrithi mumewe katika uongozi wa nchi.

Suala la kumrithi Robert Mugabe kwenye uongozi wa nchi limekua likizua mjadala mkubwa nchini Zimbabwe na kusababisha malumbano ya ndani ya chama tawala cha Zanu-PF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.