Pata taarifa kuu
LIBERIA-UCHAGUZI-SIASA

Tume ya uchaguzi Liberia yanyooshewa kidole cha lawama

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Liberia Charles Brumskine amekwenda Mahakamani kutaka Makamishena wa Tume ya Uchaguzi kuondolewa kazini.

Charles Brumskine, wakili na aliyekua mgombe akatika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais Liberia.
Charles Brumskine, wakili na aliyekua mgombe akatika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais Liberia. REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa chama cha Liberty aliyeibuka wa tatu katika mzunguko wa kwanza wa Uchaguzi wa urais mwezi Oktoba, amesema Makamishena hao walihusika na wizi wa kura.

Aidha, amesisitiza kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jerome Korkoya, na wenzake wamekosa uaminifu wa kusimamia Uchaguzi utakaokuwa huru na haki.

Mbali na kutaka Makamishena hao kuondolewa, kesi yake katika Mahakama ya Juu, kupinga matokeo ya urais ilikubaliwa na Majaji.

Majaji wa Mahakamahiyo wanaanza kusikiliza kesi ya kulalamikia madai ya vyama vitatu kuhusu matokeo ya uchaguzi huo wa kwanza, kuelekea marudi ya ya pili wiki ijayo.

Mahakama imewataka viongozi wa Tume ya Uchaguzi kujitetea dhidi ya madai hayo kabla ya kutoa uamuzi wa iwapo, kulikuwa na wizi wa kura au la, lakini pia iwapo Uchaguzi wa marudio kati ya George Weah na Makamu wa rais Joseph Boakai utaendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.