Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-ZONGO-HAKI

Burkina Faso: Tutaomba kurejeshwa nyumbani kwa François Compaoré

Serikali ya Burkina Faso imesema itaomba kurejeshwa nchini humo kwa François Compaoré, kaka wa rais wa zamani wa nchi hiyo Blaise Compaore aliezuiliwa nchini Ufaransa kufuatia uchunguzi wa kifo cha mwandishi wa habari Norbert Zongo mwaka 1998.

Zongo aliuawa mwaka 1998 akiwa anaendesha uchunguzi kuhusiana na kifo cha David Ouédraogo,dereva wa François Compaoré ndugu wa aliyekuwa rais Blaise Compaore.
Zongo aliuawa mwaka 1998 akiwa anaendesha uchunguzi kuhusiana na kifo cha David Ouédraogo,dereva wa François Compaoré ndugu wa aliyekuwa rais Blaise Compaore. AFP/Ahmed Ouoba
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Sheria nchini wa Burkina Faso, René Bagoro, ameviambia vyombo vya habari kwamba tayari barua imeandikwa kuelekea nchini Ufaransa kuwaomba viongozi wa Ufaransa kumrejesha mtuhumiwa huyo ili ahukumiwe nyumbani.

Wakili wa François Compaoré, Pierre Olivier amesema kwa sasa mteja wake yupo huru licha ya kwamba hawezi kuondoka nchini Ufaransa, wanachosubiri ni serikali ya Burkinafaso kueleza anarejeshwa nchini humo kwa misingi gani.

François Compaoré, kaka wa rais wa zamani wa Burkina Faso Blaise Compaoré, alikamatwa siku ya Jumapili asubuhi Octoba 29 katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle jijini Paris, kwa mujibu wa wakili wake, Pierre-Olivier Sur Sur.

Hati ya kimataifa ya kukamatwa ilitolewa na mahakama ya Burkina Faso kuhusiana na uchunguzi juu ya mauaji ya mwandishi wa habari Norbert Zongo mwaka 1998.

Mwili wa mwandishi wa habari Norbert Zongo na wenzake watatu ulikutwa umechomwa moto ndani ya gari mnamo mwezi Desemba mwaka 1998 wakati alikuwa akifanya uchunguzi kuhusu kifo cha David Ouedraogo, dereva wa François Compaoré.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.