Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI-SIASA

Nikki Haley aondoka DRC baada ya ziara muhimu

Balozi wa Marekani katika Baraza la Usalama la Umoja wa Umoka wa Mataifa, Nikki Haley ameondoka nchini DRC baada ya kushinikiza kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Balozi wa Marekani kwenya Umoja wa Mataifa Nikki Haley na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (CENI) Corneille Nangaa  Kinshasa Oktoba 27, 2017.
Balozi wa Marekani kwenya Umoja wa Mataifa Nikki Haley na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (CENI) Corneille Nangaa Kinshasa Oktoba 27, 2017. REUTERS/Robert Carrubba
Matangazo ya kibiashara

Balozi huyo wa Marekani Nikki Halley amesema kuna haja kwamba uchaguzi ufanyike mwaka ujao kinyume na ambavyo Tume ya uchaguzi CENI ilivyotangaza, kauli ambayo aliitoa punde baada ya kukutana na Mwenyekiti wa tume hiyo Corneille Nangaa mjini Kinshasa siku ya Ijumaa ya oktoba27

“Ni mwili muhimu kwa utaratibu wa uchaguzi. Ilikuwa wazi. Tumeonyesha kuwa siku zote ambazo uchaguzi haukupangwa, ni wanawake ndio wamebakwa, watoto ambao wamejiunga katika vikundi vya silaha. Ni muhimu kuandaa uchaguzi mwaka 2018. Ikiwa uchaguzi haukuandaliwa mwaka wa huo , DRC haitapata tena msaada wa jumuiya ya kimataifa na Marekani”

Lambert Mende, msemaji wa serikali, ameomba upinzani wa DR Congo kutolinganisha ziara ya Nikki Haley kwa "tishio. Waziri wa Mawasiliano na Vyombo vya Habari anaona "sahihi" kifungu cha mjumbe maalum wa Trump ambaye alikutana na watu mbalimbali wa DRC.

“Ilikuwa ziara sahihi sana. Hakuja kutishia watu hapa. Wapinzani lazima waelewe kuwa matatizo ya DR Congo yatakuwa na suluhisho kutoka kwa Wakongomani peke yao.Aliyo yasema ni maoni yake na uamuzi ni wa raia wa DR Congo . Ni CENI ambayo inaandaa uchaguzi. Tusubiri mpaka iweza kuchapisha kalenda ya uchaguzi”

Ifahamike pia balozi huyo alipongeza Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki, kwa kazi kubwa ya kuwapatanisha wanasiasa hadi kufikia makubaliano ya Desemba 31. Wakati huo huo Katibu mkuu wa CENCO ameeleza tangazo lao akiomba Nikky Haley kuhakiisha ya kwamba Joseph Kabila hawanii katika uchaguzi ujao.

« Kulikuwa na mazungumuzo kati yetu , Maaskofu wanasubiri kutoka jumuiya ya kimatifa msaada kwa matarajio ya raia na kila mtu anajua kwamba uchaguzi unasubiriwa kwa muda uliopangwa”

Wakati wa ziara yake DRC, balozi wa Nikki Haley alikutana pia na Rais Joseph Kabila, upinzani na Katibu Mkuu wa vyama vinavyomuunga mkono Rais Joseph Kabila akiomba kwa yote uchaguzi ufanyike .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.