Pata taarifa kuu
KENYA

IEBC yakabiliwa na maswali kuhusu idadi ya kura za urais alizopata mgombea wa Jubilee

Tume huru ya Uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC jana Jumamosi imekabiliwa na maswali magumu kuhusu hesabu ya idadi ya kura za rais wakati huu ikikimbizana na muda kukamilisha zoezi la kuthibitisha taarifa kutoka vituo vya kupigia kura na majimbo ya nchi nzima.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Mkanganyiko kuhusu idadi ya kura alizopata mgombea wa chama cha Jubilee Rais Uhuru Kenyatta na idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ni suala ambalo limedhihirika ndani ya tume hiyo.(IEBC).

Katika taarifa yake Alhamisi usiku , mweyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alisema idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ni asilimia 48 wakati vituo vya kupigia kura vilipofungwa hata hivyo saa chache baadaye Chebukati alibadili takwimu hizo na kusema idadi ya waliojitokeza kupiga kura ni karibu asilimia 34.

Hapo jana Kwa mujibu wa IEBC  rais Kenyatta anaongoza kwa asilimia 98 ya kura,huku mpinzani wake Raila Odinga ambaye alisusia uchaguzi huo anaonekana amepata kura elfu 19 na kwamba idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi huo wa marudio katika majimbo 76 ni sawa na asilimia 45.47.

 

Hata hivyo idadi ya watu waliojitokeza kwneye uchaguzi huu inaelekea kuwa ndogo zaidi kuwaho kushuhudiwa kwenye uchaguzi wa Kenya hali inayozua maswali ya kisheria kuhusu uhalali wa uchaguzi wenyewe ambao ni wazi umewagawa wananchi wa Kenya.

 

Haya yanajiri wakati ambapo kwenye miji ambayo inaelezwa kuwa ngome ya mgombea wa upinzani Raila Odinga kumeshuhuidwa vurugu kubwa ambako mamia ya watu wemejeruhiwa na baadhi yao kupoteza maisha walipokuwa wakikabiliana na polisi.

 

Maeno yaliyoshuhudiwa vurugu ni pamoja na Kisumu, Homa Bay, Migori, Siaya, Kibera, Mathare na Kawangware.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.