Pata taarifa kuu
SOMALIA-USALAMA

Rais wa Somalia atangaza vita dhidi ya Al Shabab

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed ametangaza vita zaidi dhidi ya kundi la kigaidi la Al Shabab. Al Shabab ni tishio sasa kwa usalama wa Somalia, kwa mujibu wa maafisa wa usalama wa Somalia.

Katika hotuba yake, Rais mpya wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo, ameahidi kuboresha usalama wa nchi na kukabiliana na kundi la Al Shabab.
Katika hotuba yake, Rais mpya wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo, ameahidi kuboresha usalama wa nchi na kukabiliana na kundi la Al Shabab. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Bw Mohamed metoa kauli hiyo baada ya kuongoza maandamano ya maelfu ya watu mjini Mogadishu kulaani shambulizi lililotokea wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu 276 na kuwaacha wengine kujeruhiwa.

Hadi sasa hakuna kundi lililojitokeza kusema lilitekeleza shambulizi hilo baya katika historia ya Somalia.

Shambulio la siku ya Jumamosi ni sambulio baya kabisa kuwahi kutokea nchini Somalia tangu Al Shabab kuanzisha mashambulizi dhidi ya maeneo mbalimbali na vikosi vya usalama miaka kadhaa iliyopita.

Maelfu ya watu wameuawa na mashambulizi ya kundi hili na wengine wengi wameyatoroka makazi yao na kukimbilia nchi jirani, hususan Kenya, Eritrea na Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.