Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/09 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/09 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Mlipuko wa bomu waua watu 30 Somalia

media Lori lililobeba vilipuzi lililipuka karibu na eneo linalotembelewa na watu wengi katikati mwa mji wa Mogadisgu, Somalia, Oktoba 14, 2017. REUTERS/Feisal Omar

Watu thelathini wameangamia na wengine wengi wamejeruhiwa katika mlipuko mkubwa wa bomu uliotokea karibu na lango kuu la hoteli lenye watu wengi katika mji mkuu wa Mogadishu nchini Somalia, kwa mujibu wa maafisa wa usalama.

Polisi wanasema kuwa watu wawili waliuawa katika mlipuko mwengine wa pili katika wilaya ya Madina katika mji mkuu wa nchi hiyo.

Mpaka sasa hakuna kundi ambalo limedai kutekeleza shambulio hilo, lakini inaaminiwa kwamba mlipuko huo ulitokea dakika chache tu baada ya lori lililoegeshwa na vilipuzi kulipuliwa karibu na lango kuu la hoteli, kwa mujibu wa polisi.

Raia wakiondoa miili ya waathirika wa shambulio la bomu lililotegwa katika gari lililotokea mbele ya hoteli kwenye eneo la biashara lenye watu wengi, katikati mwa Mogadishu tarehe 14 Oktoba 2017. REUTERS/Feisal Omar

Mashambulizi mengi ya kundi la Al Shabab yamekua yakiulenga mji wa Mogadishu.

Baadhi ya mashahidi wanasema kuwa hoteli ya Safari ilianguka huku watu kadhaa wakidaiwa kukwama chini ya vifusi vyake, wakiongeza kuwa wanaamni kuwa watu wengi waliangamia katika mlipuko huo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana