Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI-SIASA

Tume ya Uchaguzi yaomba kuongezewa muda kwa kuandaa uchaguzi DRC

Tume ya Uchaguzi nchini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Cono (DRC) imeomba kuongezewa muda kwa kuandaa uchaguzi, na kubaini kwamba ni vem auchaguzi huo ufanyike hadi mwezi Aprili mwaka 2019.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi DRC (CENI) Corneille Nangaa  Yobeluo (kushoto).
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi DRC (CENI) Corneille Nangaa Yobeluo (kushoto). MONUSCO/Alain Wandimoyi
Matangazo ya kibiashara

Tume ya uchaguzi (CENI) inasema inahitaji muda zaidi kuiweka sawa orodha ya wapiga kura.

Hoja hiyo imefutiliwa mbali na upinzani ukidai kwamba ni mbinu za tume hiyo kutaka kumbakiza madarakani rais Joseph Kabila ambaye muhula wake ulimalizika tangu Desemba mwaka jana,

Tume ya uchaguzi nchini DRC, katika taarifa yake, imesema inahitaji takriban siku 504 kuweza kuandaa uchaguzi wa kuaminika na wa wazi mara tu baada ya zoezi la kusajili wapiga kura litakapokamilika.

Katika makubaliano kati ya Rais Joseph Kabila na upinzani, chini ya upatanishi wa Kanisa Katoliki pande zote ziliafikiana kwamba uchaguzi ungefanyika kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Mapema mwezi Oktoba mwaka jana Mahakama ya kikatiba nchini DRC iliidhinisha ilichukua uamuzi wa kuahirisha uchaguzi wa urais kutoka Novemba mwaka huu hadi mwaka 2018, uamuzi ambao ulipingwa vikali na aliyekua waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa wakati huo, Jean-Marc Ayrault, akibaini kwamba "kuahirisha uchaguzi hadi katika tarehe isiyo ya hakika 2018 sio suluhu. Kuna hatari ya kuzuka maandamano ya fujo na ukandamizaji:, huku akiongoze kuwa "kuna njia moja pekee kutoka katika mzozo huu, na hiyo ni kuwa Rais aitishe uchaguzi na asiwanie".

Uchaguzi ulipangwa kufanyika Novemba mwaka 2016, lakini ukafutwa na tume ya uchaguzi kutokana changamoto za usafiri na za kifedha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.