Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/09 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/09 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Mwanamuziki Nyota wa Nigeria Davido ahojiwa na polisi

media Davido Mwanamuziki wa Nigeria Davido davido

Mwanamuziki Nyota wa Nigeria David Adedeji Adeleke maharufu kama Davido, amesikilizwa kwa mara nyingine tena hapo jana na Polisi ya jimbo la Lagos nchini Nigeria kufuatia kesi tata wa vifo vya watu watatu mfululizo ambao ni watu wake wa karibu waliouawa kwa kipindi cha majuma matatu ya kufuatana.

Tagbo Umeike mwenye umri wa miaka 35, alifikishwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Octoba 3 mapema alfajiri ambapo duru za polisi zinaeleza kwamba alipoteza maisha baada ya kutimia kilevi kikali aina ya Tequila kupita kiasi wakati wakiwa na mwanamuziki Davido.

Tukio hili lilizua hisi mbalimbali miongoni mwa watu wakiwemo mashabiki wa mwanamuziki huyo mwenye kujikusanyia watu milioni 2.8 kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na Milioni 5 kwenye matandao wa Instagram.

Mpenzi wa jamaa alipoteza maisha Caroline Danjuma muigizaji wa filamu nchini Nigeria alimthumu Davido kwa kumtelekeza rafiki yake.

Akizungumza na vyombo vya habari haopo jana jumatano, mkuu wa Polisi jijini Lagos Imohimi Edgal amesema Davido amejitetea mbele ya Polisi kwamba aliendelea na sherehe katika klabu baada ya tukio hilo na alipewa taarifa za kifo cha Tagbo muda mrefu baadae.

Hata hivyo mkuu huyo wa polisi amesema uchunguzi unaonyesha kwamba ni dereva wa gari Toyota Hilux iliopo kwenye mara kwa mara kwenye misafara ya Davido ndio ilioupeleka muili wa Tagbo katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospital.

Ripoti ya Hospital ya uchunguzi wa muili inaeleza kwamba alipoteza maisha baada ya kukosa hewa.

Wakati huo huo vifo vingine vya watu wawili waliuawa katika mazingira ya kutatanisha vimetokea katika watu wa karibu na mwanamuziki huyo. Maiti za watu wawili jamaa zake ziliokotwa Octoba 7 ndani ya gari aina ya BMW iliokuwa imepaki katika nyumba moja ya kifahari ilipo katika eneo la Banana Island jijini Lagos.

Vyombo vya habari jimboni hapo vilieleza kuwa vifo hivyo vimetokana na kutumia kilevi kupita kiasi, lakini polisi inasema inasubiri vipimo vya Hospital kabla ya kutoa maelezo yoyote.

Hapo jana usiku Davido alijitokeza pitia mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo ametuhumu kile alichokiita kuwa uongo unaosambazwa dhidi yake kwenye mitandao na kuhusu kuhojiwa kwake na vyombo vya dola.

Amesema kwa heshima ya Tagbo na faimilia yake hakuweza kuongea lolote tangu kutoka kifo cha rafiki yake huyo, lakini hivi karibuni ataongea na kutoa kuchapisha picha, na kwamba amechoshwa na kinachoendelea dhidi yake.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana