Pata taarifa kuu
LIBERIA-UCHAGUZi-SIASA

Wananchi wa Liberia wanamchagua rais wao mpya

Wananchi wa Liberia wanamchagua rais wao mpya Jumanne hii Oktoba 10 baada Ellen Johnson Sirleaf kumaliza muda wake wa mihula miwili. Wagombea wanaowania katika uchaguzi huo wa urais ni 20, lakini wawili au watatu pekee ndio wana ushindani mkubwa.

Mjini Monrovia, bango linalotoa wito kwa uchaguzi wenye utulivu nchini Liberia kufanyika Jumanne, Oktoba 10, 2017.
Mjini Monrovia, bango linalotoa wito kwa uchaguzi wenye utulivu nchini Liberia kufanyika Jumanne, Oktoba 10, 2017. Zoom DOSSO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo duru mbili ndio zitaamua ushindi wa rais mpya wa nchi hiyo. Uchaguzi huu ni wa kihistoria ambao ambapo itakua mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe utawala unakabidhiwa kwa njia ya kidemokrasia kutoka kwa rais anayemaliza muda wake akimkabidhi rais aliyechaguliwa.

Wapiga kura milioni 2.2 wenye umri wa kupiga kura kwa jumla ya wananchi milioni 4.6 watapiga kura leo Jumanne kuwachagua viongozi wapya mbalimbali. Watawachagua wabunge na rais wao mpya, ambaye atachukua nafasi ya Ellen Johnson Sirleaf kwa kukalia kiti cha urais katika ikulu ya Executive Mansion, mjini Monrovia.

Wagombea wakuu katika uchauguzi wa urais ni Joseph Nyumah Boakai, Charles Brumskine, Alexander Cummings, Benoni Urey na George Weah.

Rais wa kwanza mwanamke Ellen Johnson Sirleaf, baada ya kuongoza miaka sita hatawania tena urais.

Akiwa nyumbani kwake, ni "Mama Ellen". Lakini nje ya mipaka ya Liberia, jina la utani la Ellen Johnson Sirleaf ni "mwanamke jasiri", anayejulikana kwa uaminifu wake na kujitolea kisiasa kama mpinzani.

Alitarajiwa kwenye usawa, mahali pa wanawake katika siasa. Lakini Sirleaf ni mwanamke wa kipekee wakati linapokuja suala la kisiasa, wanasema wapinzani wake. Ili kuelewa tabia yake vizuri, inabidi kutazama alioyafanya hapo awali, kabla hajaingia katika ukumbi wa siasa. Akiwa na umri wa miaka 9, alimwambia bibi yake: "Nitayarishe ngao, kwa minajili ya kupambana. "

Ellen Johnson aliolewa na John Sirleaf akiwa na umri wa miaka 17. Ellen Johnson alimwambia mumewe mtarajiwa "ndiyo" nakubali, kwa mazuri na mabaya. Yeye alikua mdogo, aliilimishwa kusoma katika mazingira mazuri. John Sirleaf (Mumewe) alikua mzee. Na hasa mlevi na mwenye vurugu.

Ellen Johnson Sirleaf atakumbukwa sana nchini Liberia. Wafuasi wake wanahakikisha kwamba alibadili sura ya Liberia. Alimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe, na kuanza ujenzi wa nchi, alitumia washirika wake wa nje, kama vile Hillary Clinton. Mwaka 2011, Ellen Johnson Sirleaf alipata Tuzo ya Amani ya Nobel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.