Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Zaidi ya watu 30 wauawa kaskazini mashariki mwa DRC

media Raia wa mji wa Beni wamekua wakiukimbia mji huo kufuatia shambulio la waasi wa Uganda wa ADF. AFP/Alain Wandimoyi

Watu wenye silaha walishambulia kundi la zaidi ya raia 30 kaskazini-mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kuua wengi wao kabla ya kupambana na jeshi la serikali, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters likiwanukuu viongozi wa kisiasa katika eneo hilo.

Eneo la Mashariki mwa DRC, ambapo kunapatikana rasilimali nyingi dunia za Coltan, zinazotumiwa kwenye simu za mkononi na bidhaa nyingine za umeme, limendelea kukabiliwa na migogoro mibaya kwa zaidi ya miaka 20.

Mashambulizi hayo yalitokea siku ya Jumamosi karibu na mji wa Beni. Ikiwa idadi ya vifo hivi itathibitishwa, itakuwa ni mauaji ya kwanza ya watu wengi katika eneo hili tangu mwanzoni mwa mwaka.

Mashafuko yalikua yamekomeshwa kaskazini-mashariki mwa DRC mwaka 2017 baada ya kuwa eneo la mauaji kadhaa ambayo yaligharimu maisha ya watu zaidi ya 800 kati ya mwaka 2014 na mwaka 2016.

Kwa mujibu wa Boris Maelezo, mbunge kutoka eneo hilo, wauaji waliojihami kwa bastola na mapanga walishambulia wasafiri waliokua wakitumia pikipiki kwenye barabara kuu nayotoka Beni, katika mkoa wa Kivu Kaskazini na nchi jirani ya Uganda.

Raia wengi waliuawa katika uvamizi huo, alisema.

Kwa mujibu wa mbunge mwingine wa eneo hilo, Albert Baliesima Kadukima, wanawake wawili waliachiwa huru na wahalifu hao walieleza kuwa wauaji hao wwalichinja watu zaidi ya kumi.

Msemaji wa jeshi Mak Hazukay alisema askari wanajaribu kuwatimua watu wenye silaha mbali na sehemu ya barabara.

Kwa mujibu wa viongozi wawili tawala na afisa mmoja wa jeshi, waasi hao ni wa kundi la ADF (Allied Democratic Forces), kundi la waasi wa Uganda wanaoendesha maovu yao katika eneo la mipaka kati ya DRC na Uganda.

Serikali ya DRC yimehusisha karibu mauaji yote ya miaka mitatu iliyopita kwa waasi wa ADF, lakini kwa mujibu wa wataalam wengine, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa, makundi kadhaa ya silaha, pamoja na wakuu wa jeshi la DRC, FARDC, ni chazo cha mauaji haya katika mfumo wa mapambano ya ushawishi katika eneo hilo.

Wakati huo huo, wafuasi wa kundi la wanamgambo Bantu wametorosha wafungwa zaidi ya hamsini kutoka jela la Pweto kusini mashariki mwa DRC, afisa wa serikali ya mitaa amesema.

Idadi kubwa ya wafunga wanaotoroka jela imeshuhudiwa katika miezi ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na kisa kimoja mjini Kinshasa, mji mkuu wa DRC, wakati ambapo wafungwa zaidi ya 4,000 walitoroka. Hali ya usalama imezorota nchini DRC tangu Rais Joseph Kabila akatae kujiuzulu baada ya muhula wake kumalizika kulingana na katiba ya nchi hiyo mwezi Desemba mwaka jana.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana