Pata taarifa kuu
TUNISIA-WAHAMIAJI_USALAMA

Tunisia: Watu wengi wapoteza maisha baada ya boti la wahamiaji kugongana na meli ya kijeshi

Meli ya kivita ya Tunisia imegongana na boti lililokua likisafirisha wahamiaji. Ripoti ya mwishoinabaini kwambawatu nane wamepotza maisha na wengine wengi hawajulikani waliko.

Wahamiaji wanasubiri kuokolewa na kikosi cha walinzi wa powani ya Italia, kilomita 30 kutoka pwani ya Libya, tarehe 6 Agosti 2017.
Wahamiaji wanasubiri kuokolewa na kikosi cha walinzi wa powani ya Italia, kilomita 30 kutoka pwani ya Libya, tarehe 6 Agosti 2017. ANGELOS TZORTZINIS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo ilitokea siku ya Jumapili jioni kilomita hamsini kutoka kisiwa cha Tunisia cha Kerkennah. Kufuatia ajali hiyo, boti lililokua likisafirisha wahamiaji wasiopungua 70, lilizama mara moja. serikali ya Tunisia imetangaza tukio hilo Jumatatu hii asubuhi, ikisema kuwa moja ya meli zake za kijeshi zilikuwa zimeona boti inayofanya safari za siri kwenye bahari ya Maediterranean, na wakati huo ilikua vigumu kuepuka ajali hiyo.

Uchunguzi na utafiti, vinavyosimamiwa na mamlaka ya Malta, vnaendelea kujaribu kupata manusura. Waathirika walikua wakitokea katika mji wa Tunisia wa Sfax.

Zaidi ya wahamiaji 4,000 waliwasili miezi miwili iliyopita katika mji wa Sicily nchini Italia.

Tunisia ina wasiwasi na idadi kubwa ya wananchi wake kati ya wahamiaji hawa. Na serikali ya Italie, ambayo iliombwa kufungwa kwa njia ya Libya ili kukomesha kuwasili kwa wahamiaji hao nchini mwake, sasa wameshindwa la kufanya kufuatia nji hii mpya kutoka Tunisia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.