Pata taarifa kuu
LIBERIA-UCHAGUZi-SIASA

Liberia yajiandalia uchaguzi wa urais siku ya Jumanne

Wapiga kura wa Liberia wapatao Milioni mbili, siku ya Jumanne wiki hii watapiga kura kumchagua rais mpya. Utakuwa ni uchaguzu wa tatu tangu mwaka 2003, baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf.
Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Rais wa kwanza mwanamke Ellen Johnson Sirleaf, baada ya kuongoza miaka sita hatawania tena urais.

Wagombea urais 20 wanawania nafasi hiyo akiwemo George Weah mchezaji wa zamani wa mchezo wa soka na mgombea pekee wa kike MacDella Cooper.

Mgombea pekee wa kike nchini Liberia. MacDella Cooper
Mgombea pekee wa kike nchini Liberia. MacDella Cooper AFP/Zoom Dosso

Rais mwanamke wa kwanza kutoka nchi za afrika kuachia ngazi

Uchaguzi wa urais nchini Liberia umepangwa kufanyika siku ya Jumanne Oktoba 10. Ellen Johnson Sirleaf, mwanamke wa kwanza aliyechaguliwa na wananchi kupitia wabunge katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, ataachia ngazi.

Akiwa nyumbani kwake, ni "Mama Ellen". Lakini nje ya mipaka ya Liberia, jina la utani la Ellen Johnson Sirleaf ni "mwanamke jasiri", anayejulikana kwa uaminifu wake na kujitolea kisiasa kama mpinzani.

Alitarajiwa kwenye usawa, mahali pa wanawake katika siasa. Lakini Sirleaf ni mwanamke wa kipekee wakati linapokuja suala la kisiasa, wanasema wapinzani wake. Ili kuelewa tabia yake vizuri, inabidi kutazama alioyafanya hapo awali, kabla hajaingia katika ukumbi wa siasa. Akiwa na umri wa miaka 9, alimwambia bibi yake: "Nitayarishe ngao, kwa minajili ya kupambana. "

Ellen Johnson aliolewa na John Sirleaf akiwa na umri wa miaka 17. Ellen Johnson alimwambia mumewe mtarajiwa "ndiyo" nakubali, kwa mazuri na mabaya. Yeye alikua mdogo, aliilimishwa kusoma katika mazingira mazuri. John Sirleaf (Mumewe) alikua mzee. Na hasa mlevi na mwenye vurugu.

Ellen Johnson Sirleaf atakumbukwa sana nchini Liberia. Wafuasi wake wanahakikisha kwamba alibadili sura ya Liberia. Alimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe, na kuanza ujenzi wa nchi, alitumia washirika wake wa nje, kama vile Hillary Clinton. Mwaka 2011, Ellen Johnson Sirleaf alipata Tuzo ya Amani ya Nobel.

George Weah mchezaji wa zamani wa mchezo wa soka awania kiyi cha urais Liberia.
George Weah mchezaji wa zamani wa mchezo wa soka awania kiyi cha urais Liberia. LA Bagnetto

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.