Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Donald Trump aombwa kuingilia kati mzozo wa kisiasa wa DRC

media Wafuasi wa upinzani katika mitaa ya mji mkuu wa Kinshasa Septemba 19, 2016. Reuters/ File

Wajumbe saba wa baraza la seneti nchini Marekani wamemuandikia barua rais Donald Trump kumtaka ajihusishe zaidi katika kutafuta suluhu ya mzozo wa Kisiasa nchini DR Congo.

Wanaseneti hao wanasema iwapo mkataba wa kisiasa wa desemba 31 mwaka jana hautotekelezwa na kukosekana kwa majibu ya kisiasa kutoka Kinshasa, vikwazo vipya dhidi ya utawala wa rais Joseph Kabila lazima vichukuliwe.

Kinshasa inasema inasubiri majibu ya rais Donald Trump ambae hivi karibuni alisema kwamba anafuatilia kwa karibu hali ya kisiasa nchini DRC, ambapo hadi sasa rais huyo hajajihusisha zaidi na siasa ya Afrika.

Katika kikao cha Umoja wa Mataifa kilichofanyika mwezi Septemba iliopita, rais Trump alieleza kuguswa na machafuko yanayoripotiwa nchini DRCongo.

Hata hivyo serikali ya DRCongo kupitia msemaji wake Lambert Mende amesema wamezoea kauli na mwenendo wa wabunge wa baraza la seneti kutoka chama cha demokrat.

Wachunguzi wa mambo wanasema rais Trump ambe amekuwa mt wa kushtukiza, hawezi kuzungumza lolote kabla ya ziara ya Nikki Haley mjumbe wa Marekani kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Octoba 21 jijini Kinshasa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana