Pata taarifa kuu
CAMEROON-HAKI-USALAMA

Makabilano kati vya polisi na vijana yanaendelea Cameroon

Polisi na wanajeshi wameendelea kupiga doria katika mitaa mbalimbali ya mikoa ya Cameroon inayozungumza lugha ya Kiingereza. Operesheni hii ya jeshi na Polisi inakuja siku mbili baada ya kutokea kwa vurugu zilizogharimu maisha ya watu siku ya Jumapili.

Makabiliano kati ya polisi na wanaharakati wanaotaka maeneo yao kujitawala yanaripotiwa kuendelea nchini Cameroon.
Makabiliano kati ya polisi na wanaharakati wanaotaka maeneo yao kujitawala yanaripotiwa kuendelea nchini Cameroon. via REUTERS TV
Matangazo ya kibiashara

Makabiliano kati ya vikosi vya usalama na wanaharakati wanaotaka mikoa yao kujitawala yalisababisha vifo vya watu zaidi ya kumi.

Kiongozi wa upinzani nchini humo, John Fru Ndi ameviambia vyombo vya habari kwamba watu 30 waliuawa katika vurugu hizo, huku akinyooshea kidole cha laawama vikosi vya usalama na ulinzi kuhusika na vurugu hizo.

Hata hivyo katika baadhi ya maeneo, hasa katika mji wa Bamenda, Kaskazini Magharibi makabiliano bado yanaendelea kati ya vijana na polisi wa kuzuia ghasia.

Polisi imekua ikitumiamabomu ya kutoa machozi kwa kuwatawanya waandamanaji.

Kwa upande wa waandamanaji wanaotaka kujitenga kwa maeneo hayo, kazi ilikuwa ngumu kuliko ilivyotarajiwa. Walitakiwa kutumia mbinu zaidi kutokana na wingi wa polisi na askari waliokua walitumwa kuzingira maeneo hayo ya Kusini-Magharibi na Kaskazini Magharibi.

Wakati nmwingine, walikabiliana na vikosi vya usalama, walipokua wakijaribu kuvunja vizuizi vya polisi, hususan kusini-magharibi kwenye kituo cha usafiri kkaribu na mji wa Limbe, ambapo makabiliano mkali yalishuhudiwa. Kwa mujibu wa mashahidi, baadi ya waandamanaji walivamia kituo cha polisi.

Ghasia hizo zimetokea wakati wa maadhimisho ya miaka miaka hamsini na sita tangu kujumuishwa kwa jimbo la wazungumzaji wa Kiingereza ndani ya Cameroon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.