Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-USALAMA

Polisi wawili wauawa katika shambulio la kuvizia kaskazini mwa Burkina Faso

Polisi wasiopungua wawili waliuawa na wengine wawili kujeruhiwa siku ya Jumanne jioni, Septemba 26, katika shambulio la kuvizia dhidi ya msafara wa malori ya mafuta ya kampuni ya madini.

Shambulio lilifanyika katika mkoa wa Soum, kaskazini mwa Burkina Faso. Hapa, ni karibu na mji wa Markoye (Picha ya zamani).
Shambulio lilifanyika katika mkoa wa Soum, kaskazini mwa Burkina Faso. Hapa, ni karibu na mji wa Markoye (Picha ya zamani). Marco Schmidt / Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lililoendeshwa na watu wenye silaha lilitokea karibu na mji wa Djibo, katika mkoa wa Soum.

Ilikua saa 10:30 alaasiri (saaa za Burkina Faso) wakati msafara wa malori ya kampuni ya madini ya Belahourou yaliyokua yakibeba mafuta yaliposhambuliwa na watu wasiojulikana.

Gari la polisi iliyokua ikiongozana na msafara huo ililipuliwa na bomu la kutegwa ardhini kwenye barabara inayotoka Tongomayel kwenda Inata, kilomita zaidi ya sitini kutoka mji wa Djibo, katika mkoa wa wa Soum. Wakati polisi na washambuliaji walirushiana risasi kwa muda wa dakika kadhaa, na baadae washambuliaji walifanikiwa kukimbia.

Askari wawili waliuawa na wengine wawili walijeruhiwa vibaya.

Mashambulizi matatu ndani kipindi kisichozidi wiki moja

Hali ya usalama kaskazini mwa Burkina Faso inaendelea kuzorota na kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama na mauaji ya ya kuvizia.

Hili ni shambulio la tatu katika mkoa huu katika kipindi kisichozidi wiki moja. Kituo cha polisi katika kambi ya wakimbizi ya Mentaoilichomwa moto siku ya Jumamosi 23 Septemba na kusababisha hasara kubwa, huku polisi saba wakijeruhiwa baada ya gari lao kulipuliwa na bomu la kutegwa ardhini, kilomita kadhaa kutoka mji wa Djibo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.