Pata taarifa kuu
CAR-UFARANSA-USHIRIKIANO-USALAMA

Macron: Jamhuri ya Afrika ya Kati inahitaji kuwa na mamlaka zenye nguvu

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemhakikishia rais wa Jamuhuri ya Afrika ya kati Faustin Ange Twadera kwamba Ufaransa itaendeleza juhudi za kusaidia upatanisho nchini mwake.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra.
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra. STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Emmanuel Macron ambae amempokea Ikulu ya Elysee rais wa Jamuhuri ya Afrika ya kati Faustin Ange Touadera kwa mara ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake amesema hali ya usalama mdogo inayoendelea kushuhudiwa nchini Jamuhiri ya Afrika ya kati lazima ishuhghulikiwe ili kufanikisha mchakato wa maridhiano.

Rais wa Ufaransa amesisitiza kwamba serikali yake inaunga mkono hatua za kuimarisha serikali, haki na vita dhidi ya rushwa ambavyo ni adui mkubwa wa maendeleo. Hata hivyo hakutoa maelezo zaidi kuhusu kauli yake hiyo.

Serikali ya rais Touadera imeshindwa kudhibiti nchi nzima na kuishia pekee katika mji mkuu Bangui ambapo maeneo mengine yanaendelea kukaliwa na makundi ya waasi huku wizi wa rasilimali ukishuhudiwa pamoja na mauaji ya hapa na pale yakiripotiwa.

Katika hatua nyingine, msemaji wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Akti (Minusca), Uwolowulakana Ikavi-Gbetanou, amearifu kuwa mwanajeshi mmoja wa kikosi cha Minusca kutoka nchini Moroco amejeruhiwa kusini mashariki mwa nchi hiyo wakati wa makabiliano na makaundi ya waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.