Pata taarifa kuu
DRC-UN-HAKI ZA BINADAMU

Visa vya ukiuwaji wa haki za binadamu vyaendelea DRC

Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema imerekodi visa zaidi ya 440 vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika mwezi Agosti peke yake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Maandamano dhidi ya kupitishwa sheria mpya ya uchaguzi, katika mji wa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Januari 19 mwaka 2015.
Maandamano dhidi ya kupitishwa sheria mpya ya uchaguzi, katika mji wa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Januari 19 mwaka 2015. AFP PHOTO/ PAPY MULONGO
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa kitengo cha haki za binadamu, Jose Maria Aranaz amewaambia waandishi wa habari kuwa idadi hii ni mara mbili zaidi ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyorekodiwa mwezi Julai.

Ripoti ya Aranaz imeonesha kuwa asilimia 64 ya vitendo vya mauaji na unyanyasaji vimetekelezwa na vyombo vya usalama vya DRC.

Hata hivyo Aranaz amepongeza hatua ambazo zimeendelea kuchukuliwa na Serikali ya DRC katika kuwashughulikia watu waliotekeleza vitendo hivi, akitolea mfano kutolewa uamuzi wa kesi zaidi ya 12 zilizowahusisha maofisa wa jeshi la Serikali katika mwezi Agosti.

Ripoti hii imetolewa wakati ambao Serikali ya Kinshasa imeendelea kukanusha kwa nguvu kuhusu vyombo vyake vya usalama kuhusika pakubwa na vitendo vya unyanyasaji wa raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.