Pata taarifa kuu
UN-DRC-MAUAJI-USALAMA

UN yajibu baada ya RFI kuweka wazi taarifa kuhusu mauaji ya wataalam wake

RFI imechapisha uchunguzi wa kipekee kuhusu mauaji ya wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa, waliouawa miezi sita iliyopita Machi 12, katika Kasai. Uchunguzi huu unatofautiana na toleo la serikali na unaonyesha njia jinsi gani wataalam hao walivofanyiwa mtego.

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (hapa akiwa Addis Ababa, Ethiopia, Januari 30, 2017)
Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (hapa akiwa Addis Ababa, Ethiopia, Januari 30, 2017) REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi huu pia unaonyesha kushindwa kwa "board of inquiry", kamati ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa. Wachunguzi waliotumwa na Umoja wa Mataifa walihitimisha toleo sawa na lile la mahakama ya kijeshi ya DRC inayonashughulikia kesi hiyo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amejibu baada ya RFI kuweka wazi taarifa kuhusu mauaji ya wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa katika mji wa Kasai mwezi Machi mwaka huu, Zaida Catalan na Michael Sharp. Ufunuo wa mwisho wa RFI hauthibitishi toleo la serikali na kuweka wazi uwezekano wa wataalam hao kufanyiwa mtego. Pia imetiliwa mashaka kushindwa kwa tume iliyoundwa na Umoja wa Mataifa, ambayo ilihitimisha kwa toleo sawa na lile la mahakama ya kijeshi ya DRC.

Kuhusu kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema bado kuna uwezekano: "Tunafanya mashauriano niliotoa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na familia ya wahanga, ili kuanzisha mfumo wetu. Kulikuwa na uwezekano tofauti. Njia bora zaidi ni kuingiza wataalam huru kwenye vyombo vya sheria vya DRC. Sijui ikiwa itawezekana au la. Ikiwa haitawezekana, tutatumia njia nyingine inayotuhusu. Wenzetu katika Idara ya Mambo ya Siasa wanafanya mashaurianoyote muhimu kutekeleza mfumo ambao unaweza kuwa kama ufanisi kama iwezekanavyo ili ukweli ujulikane. "

Siku ya Jumatano Ufaransa ulielezea kuwa iko tayari kwa mfumo wa uchunguzi maalum utakaotoa mwanga juu ya mauaji hayo. Na nchini DRC, Waziri wa Mawasiliano, Lambert Mende, anahoji umuhimu wa uchunguzi huu. "Si kwa serikali wala kwa vyombo vya habari kutaja mshutmiwa badala ya majaji," alisema msemaji wa serikali, ambaye amesema kesi iko mbele ya mahakama ya kijeshi katika mji wa Kananga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.