Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

UN yalaani udhalimu unaofanyiwa watoto na vijana wanapoelekea Ulaya

media Boti linalobeba wahamiaji ikisubiri upwa msaada meli ya "Aquarius" ya SOS Méditerranée na MSF kwenye pwani ya Libya Agosti 2, 2017. Tangu wakati huo, mashirika yasiyo ya kiserikali yamekatazwa kutumia pwani ya Libya. Angelos Tzortzinis / AFP

Umoja wa Mataifa umesema kuwa robo tatu ya watoto na vijana wanaojaribu kukimbilia barani Ulaya ni wahanga wa vitendo vya mateso, ubakaji na matukio mengine ya unyanyasaji wakati wanapofanya safara ya hatari kuingia Ulaya.

Maofisa kutoka shirika la umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNCEF na lile linalohusika na wahamiaji IOM wanasema kuwa wahamiaji wengi vijana hasa kutoka kwenye nchi za kusini mwa jangwa la Sahara ndio wako hatarini zaidi kufanyiwa vitendo hivi.

Akizungumza na wanahabari mjini Brussels, mkurugenzi wa UNICEF Sandie Blanchet amesema vijana wengi waliohojiwa wameeleza namna wanavyofanyiwa vitendo vya kinyama.

Kwenye ripoti yake UNICEF inasema kuwa asilimia 77 ya watoto na vijana wanaojaribu kuvuka bahari ya Mediterania kuingia Ulaya wamefanyiwa vitendo vya unyanyasaji ambavyo vingi vimechangia kukithiri kwa biashara haramu ya binadamu.

UNICEF inasema vijana wanaotoka kwenye nchi za jangwa la Sahara ndio wako hatarini zaidi kuliko wanaotoka kwenye maeneo mengine.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana