Pata taarifa kuu

Mmoja wa watuhumiwa wa mauaji ya wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa, DRC, atambuliwa

Miezi sita iliyopita, wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa walitoweka katika Kasai ya Kati. Miili ya Michael Sharp na Zaida Catalan ilipatikana wiki mbili baadaye. Mpaka sasa hakuna taarifa za makalimani wao wawili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kesi inaendelea Kananga, mji mkuu wa mkoa wa Kasai.

Wataalam wa Umoja wa Mataifa Zaida Kikatalani (picha ya mwaka 2009) na Michael Sharp waliuawa Kasaï mnamo Machi 2017.
Wataalam wa Umoja wa Mataifa Zaida Kikatalani (picha ya mwaka 2009) na Michael Sharp waliuawa Kasaï mnamo Machi 2017. BERTIL ERICSON, TIMO MUELLER / TT News Agency / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wanamgambo wa Kamuina Nsapu ambao mahakama ya kijeshi ya DRC inashtumu kuhusika na mauaji hayo wanaendelea kushikiliwa. Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa walihitimisha toleo sawa na lile la mahakama ya kijeshi ya DRC inayoshughulikia kesi hii. Lakini miezi sita baada ya mauaji hayo, uhalifu usiokuwa wa kawaida nchini DRC, RFI inachapisha uchunguzi wa kipekee ambao unatia shaka juu ya toleo la serikali na kuonyesha njia nyingine ambayo inawezekana kuwa ndio sahihi.

RFI imepata sauti iliyorekodiwa kati ya wataalamu hao na wafuasi wa kiongozi wa kijadi kwenye eneo hilo Kamuina Nsapu, mkutano ambao uliingiliwa na maofisa wa serikali waliodaiwa kuwapotosha wataalamu hao.

Michael Sharp na Zaida Catalan walikua na ahadi ya kukutana na mmoja kati ya wajumbe wa mahakama ya Kamuina Nsapu ambao walikuja kujadili makubaliano na serikali ya DRC. Wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa, waliandaa safari kewnda katika kijiji cha Bunkonde, ambako walitarajia kujua zaidi kuhusu makundi ya wanamgambo wenye silaha "tofauti sana" na kile wanachokijua kuhusu Kamuina Nsapu.

Mkalimani mmoja wa wataalamu wawili hazungumzi Kifaransa. Kwa mara kadhaa aliwaonya wataalam hao wawili dhidi kutokwenda Bunkonde na kuwaomba kuwa wanapaswa kwenda katika kijiji cha Kamuina Nsapu, ambako alifikiri angeweza kudhibiti wanamgambo. Lakini kamwe maonyo haya katika lugha ya Ciluba, lugha inayozungumzwa Kasai, hayakutatafsiriwa. Hatua zote za usalama zilitolewa. Na miongoni mwa wale waliowatapeli wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa, RFI imeweza kutambua mkalimani wao: Betu Tshintela ambaye aliongozana nao, binamu yake José Tshibuabua, afisa wa idara ya ujasusi (ANR). Na mwanachama wa familia ya kifalme, aliye karibu na kiongozi mpya, Thomas Nkashama ambaye aliweka kwenye kitambulisho chake na kujiita Tom Perriello, jina la mjumbe maalumu wa zamani wa Marekani. Kwa mujibu wandugu wa mashahidi, Thomas Nkashama kwa sasa ni afisa wa idara nyingine ya usalama ya DRC, DGM.

Serikali ya DRC ilisema baada ya kuuawa kwa wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa kwamba haikufahamishwa kuhusu safari ya wataalamu hao kwenda Bunkonde. Thomas Nkashama na José Tshibuabua kamwe hawajafikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi mjini Kananga. Wote walikuwa hawapatikani katika siku chache zilizopita.

Shahidi mkuu wa mauaji hayo ni mpelelezi wa jeshi la DRC, kiongozi wa wapiganaji wa ziada wa FARDC, wanasema wakazi wa Bunkonde, madai ambayo Jean Bosco Mukanda anakanusha. Jean Bosco Mukanda ndio ambaye alionyesha kaburi la wataalamu hawa wawili waliouawa. Na yeye ndio ambaye aliwataja watuhumiwa ambao wanazuiliwa leo.

Mbele ya mahakama, shahidi huyu alisema alishuhudia mauaji ya wataalam hao, huku akihakikishia kuwa alikuwa amekwisha uawa mwezi mmoja kabla na wanamgambo hao hao lakini ambao siku hiyo hakuwa na wasiwasi nao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.