Pata taarifa kuu
DRCONGO

Shirika la afya WHO latahadharisha juu ya mlipuko wa kipindupindu DRC

Shirika la afya la kimataifa WHO limetoa tahadhari juu ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindu pindu nchini Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo ambao hadi sasa umegharimu maisha ya watu 528 kiwango kinachotishia zaidi.

Wahamasishaji wa kijamii mjini Kinshasa, RD Congo wakibandika matangazo ya tahadhari dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu
Wahamasishaji wa kijamii mjini Kinshasa, RD Congo wakibandika matangazo ya tahadhari dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu Photo OMS/Eugene Kabambi
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika hilo ugonjwa wa kipindupindu umekuwa tatizo nchini humo baada ya kushuhudia ripoti za mamilioni ya raia wakiugua nchini humo kila mwaka na idadi ya vifo kufika mia nane na kumi na saba.

Taarifa ya umoja wa mataifa inasema mlipuko wa Ebola nchini DRC imefikia hali mbaya katika majimbo 20 kati ya 26 yameathirika na ugonjwa huu.

Kulingana na takwimu za WHO kuna waathirika kati ya milioni moja nukta nne na milioni nne nukta tatu duniani kila mwaka na vifo takribani laki moja na elfu arobaini na mbili.

Mnamo september 2 mamlaka nchini DRC imerekodi visa elfu ishirini na nne mia mbili na kumi na saba.

Mlipuko huo umeathiri miji kadhaa mashariki,magharibi kasazini na maeneo ya jiji kuu la Kinshasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.