Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-EFF-DA-USHIRIKIANO-SIASA

Muungano kati ya EFF na DA kuvunjika Afrika Kusini

Ni mwaka mmoja sasa tangu chama cha DA kupata ushindi mkubwa ktika miji ya Pretoria, Johannesburg na Port Elizabeth, kupitia uchaguzi wa kihistoria wa manispaa.

Julius Malema, kiongozi wa chama cha EFF (kulia) ametuma ujumbe mkali kwa washirika wake wa zamani wa DA
Julius Malema, kiongozi wa chama cha EFF (kulia) ametuma ujumbe mkali kwa washirika wake wa zamani wa DA REUTERS/Siphiwe Sibek
Matangazo ya kibiashara

Ili kuongoza katika miji hii mikubwa mitatu, chama cha DA kiilitakiwa kujiunga na chama cha EFF cha Julius Malema ili kupata idadi kubwa kabisa ya viti dhidi ya chama tawala cha ANC, ambacho kiliongoza katika uchaguzi huo lakini kwa kura ya chini ya 50% katika baadhi ya miji.

Mwaka mmoja baadaye, uhusiano huu kati ya vyama hivi viwili vya upinzani DA na EFF umeanza kuvunjika wakati ambapo Julius Malema ametangaza kujitenga na chama hicho.

 

Chama cha DA kinakabiliwa na hali ngumu wiki hii, na hasa kutengwa katika ngazi ya taifa na bungeni. Ikiwa hakijakubaliana na vyama vingine vya upinzani, chama hiki kinaweza hata kupoteza udhibiti wa Pretoria, Johannesburg na Port Elizabeth.

Chama cha EFF cha Julius Malema kimejawa na ghadhabu, tangu chama cha DA kilipomfuta kazi naibu meya wa mji wa Port Elizabeth, mfuasi wa chama cha UDM, kwa kushtumiwa kupiga kura na chama cha ANC wakati wa kikao cha halmashauri ya manispaa. Kufuatia kufukuzwa kwa kiongozi huo, chama cha EFF kiliamua kususia vikao vya halmashauri za manispaa katika miji mitatu mikubwa inayoongozwa na chama cha Democratic Alliance (DA).

Julius Malema ametuma ujumbe mkali kwa washirika wake wa zamani. "Upigaji kura wetu kwa kuunga mkono chama cha DA hautafatishwa tena. Tutapiga kura kulingana na kile watakachoweka mezani. Ikiwa ANC itatoa pendekezo zuri, tutapiga kura pamoja nao. Hatuko marafiki wa chama chenye wazungu wengi. Ikiwa ndivyo ilivyokuwa, tungelijiunga pamoja nao, tungekuwa tumesaini makubaliano, lakini hatukusaini chochote. "

Kufuatia kususia huo kwa chama cha EFF, kikako cha mwisho cha halmashauri ya jiji la Pretoria kimeahirishwa kwa kukosa idadi kubwa ya wajumbe. Kama mambo hayatabadilika, chama cha ANC kinaandaa kura ya kutokua kwa lengo la kumuangusha Herman Mashaba, Meya wa Johannesburg kutoka chama cha DA.

Mmusi Maimane amesema kuwa mazungumzo bado yanawezekana. Ameomba wajumbe wa vyama vya EFF na UDM kukutana kwa haraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.