Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Amnesty International: Boko Haram yaua watu 400 tangu mwezi Aprili

media Jiji la Maiduguri na viunga vyake, kaskazini mashariki mwa Nigeriaumekua ukilengwa na mashambulizi ya Boko Haram (hapa ni baada ya shambulio la Machi 15 2017). STRINGER / AFP

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Amnesty International linasema kuwa kundi la Boko Haram limewauwa watu 400 tangu mwezi Aprili mwaka huu.

Amnesty International inasema mauaji mengi yametekelezwa nchini Nigeria na Cameroon, na idadi hii ni mara mbili ikilinganishwa na miezi mitano iliyopita.

Ripoti ya Shirika hilo inaeleza kuwa, wasichana wadogo walitumiwa na kundi hilo kutekeleza mauaji hayo kwa kujilipua baada ya kufungwa mabomu mwilini.

Mauaji haya yameelezwa na Amnesty International kama ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na vita vya uhalifu.

Tangu kuanza kutekeleza mashambulizi mwaka 2009, raia watu 20,000 wameuawa nchini Nigeria na nchi jirani huku wengine Milioni 2.6 wakiyakimbia makwao.

Amnesty International inataka Jumuiya ya Kimataifa kufanya zaidi kushinda kundi hili.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana