Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-SIASA

Wek Ateny: Salva Kiir hana nia ya kuachia ngazi

Msemaji wa rais Salva Kiir amesema kuwa kiongozi huyo hana nia yoyote ya kung’atuka madarakani kama kiongozi wa taifa la Sudan Kusini.

Rais wa Sudan Kusini  Salva Kiir.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir. REUTERS/Jok Solomun
Matangazo ya kibiashara

Ateny Wek Ateny amesema haya katika taarifa iliyotolewa hapo jana kwa uma ikisisitiza kuwa rais Salva Kiir hajapanga kuondoka madarakani ili kumpisha aliyewahi kuwa mshauri wa zamani wa rais Costello Garang Riiny Lual.

Katika hatua nyingine maofisa wa waasi nchini humo wameendelea na juhudi za kuwashirikisha viongozi wa ukanda ili kusaidia kurejea nyumbani kwa kiongozi wao Riek Machar aliyeko nchini Afrika Kusini.

Machar kwa muda sasa wamezuiliwa kutoka nchini Afrika Kusini toka alipokimbilia huko baada ya kujeruhiwa akitokea Khartoum mwaka mmoja uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.