Pata taarifa kuu
CAMEROON-HAKI

Paul Biya: Naachana na mashitaka dhidi ya viongozi wa maandamano

Rais wa Cameroon Paul Biya ametangaza kufutwa kwa mashtaka dhidi ya viongozi wa wananchi wa kaskazini magharibi na kusini magharibi mwa nchi hiyo, maeneo ambayo lugha inayozungumzwa ni Kingereza.

Paul Biya, Rais wa Cameroon aamua kuachana na mashitaka dhidi ya wanaharakati kutoka maeneo yanayozungumza Kiingereza, Cameroon.
Paul Biya, Rais wa Cameroon aamua kuachana na mashitaka dhidi ya wanaharakati kutoka maeneo yanayozungumza Kiingereza, Cameroon. AFP PHOTO / REINNIER KAZE
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati hao walioachiliwa huru ni pamoja na Nkongho Agbor Félix, Fontem Aforteka'a Neba, Paul Ayah Abine pamoja na wale wote waliokamatwa kufuatia vurugu na maandamano ya hivi karibuni kudai kutengwa na serikali.

Msemaji wa serikali ya Cameroon Issa Tchiroma-Bakary, amesema hatuwa hiyo ya rais Biya ni ya kupongezwa.

Joto la kisiasa lilikuwa liemanza kushika kasi katika miji ya Bamenda, kaskazini magharibi na Buya, Kusini magharibi ambako wananchi wanazungumza Kingereza wakionekana kupinga serikali ya nchi hiyo hadi kuanza harakati za kuomba mjitengo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.