Pata taarifa kuu
TOGO-SIASA-USALAMA

Upinzani kusitisha maandamano dhidi ya serikali Togo

Muungano wa vyama vya upinzani nchini Togo umetangaza kusitisha maandamano yao dhidi ya Serikali lakini umesisitiza kuachiwa huru kwa waandamanaji waliokamtwa wakati wa maandamano ya Agosti 19 na 20 mwaka huu.

Vikosi vya usalama vya Togo vikijaribu kuwasambaratisha wafuasi wa upinzani katika mji mkuu wa Lome tarehe 22 Agosti 2012.
Vikosi vya usalama vya Togo vikijaribu kuwasambaratisha wafuasi wa upinzani katika mji mkuu wa Lome tarehe 22 Agosti 2012. AFP/EMILE KOUTON
Matangazo ya kibiashara

Maandamano ya awamu ya pili ya upinzani yaliyokuwa yamepangwa kufanyika Agosti 30 na 31 ya mwezi huu yametangazwa kuahirishwa hapo jana na muungano wa vyama sita na sasa yamepangwa kufanyika Septemba 6 na 7 ya mwezi ujao.

Taarifa ya muungano wa vyama hivyo imesema kuwa kuahirishwa kwa maandamano ya mwisho wa mwezi huu kunalenga kuishirikisha nchi nzima katika maandamano hayo ya kutaka kufanyika marekebisho ya katiba ya mwaka 1992 na kumalizika kwa utawala wa Gnassingbe.

Vyama hivyo pia vimewataka wafuasi wao kujitokeza kwa uwingi leo asubuhi katika mahakama kuu ya mjini Lome ambako wenzao zaidi ya 27 waliokamtwa kwenye maandamano ya awali watakuwa wanapandishwa kizimbani.

Jumla ya watu 7 waliuawa katika maandamano ya juma moja lililopita mjini Lome.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.