Pata taarifa kuu
ULAYA-AFRIKA-WAHAMIAJI

Ulaya-Afrika: Macron atoa mpango wa hatua kwa wahamiaji

Viongozi wa bara la Afrika na Ulaya wamekubaliana kuzuia maelfu ya wahamiaji kutoka barani Afrika kutumia bahari ya Meditterraean kwenda barani Ulaya.

Mkuu wa Mashauri ya Kigeni ya Ulaya Federica Mogherini, Marais wa Nigeria Mahamadou Issoufou, wa Chad Idriss Deby, wa ufaransa Emmanuel Macron, wa Ujerumani Kansela Angela Merkel na Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy, mjini Paris tarehe 28 Agosti.
Mkuu wa Mashauri ya Kigeni ya Ulaya Federica Mogherini, Marais wa Nigeria Mahamadou Issoufou, wa Chad Idriss Deby, wa ufaransa Emmanuel Macron, wa Ujerumani Kansela Angela Merkel na Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy, mjini Paris tarehe 28 Agosti. ludovic MARIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, imekubaliwa kuwa vituo maalum vitawekwa nchini Niger na Chad, hasa wale wanotaka kupewa hifadhi na Umoja wa Mataifa.

Maelfu ya wahamiaji wamekuwa wakihatarisha maisha yao kuvuka bahari ya Mediterranean kwenda barani Ulaya.

Maelfu ya wahamiaji wamekuwa wakihatarisha maisha yao kuvuka bahari ya Mediterranean kwenda barani Ulaya.

Swala kubwa ikiwa ni kupanga mikakati ya kukabiliana na wahamiaji haramu kuanzia kwenye mizizi yake.

Rais wa ufaransa Emmanuel Macron ambaye alikuwa mwenyeji wa mkutano huo, alisema nchi yake pamoja na Ulaya watazidisha ushirikiano na mataifa wanakotoka wahamiaji hao.

Rais wa Niger Mahamadu Issoufou alieleza kufurahishwa na mpango huo pamoja na ushirikiano wanaopewa.

Kwa upande wake rais wa Tchad Idriss Deby Itno alisema ni muhimu kumaliza tatizo hilo moja kwa moja.

Watu 140.000 wamepoteza maisha katika bahari ya Mediteranian tangua mwaka 2014 wakati wakijaribu kusafiri kuelekea barani Ulaya kuomba hifadhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.