Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-AFRIKA KUSINI-GRACE

Mugabe ashambulia wazungu Afrika Kusini

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amewajia juu wazungu walioko nchini Afrika Kusini, akihoji ni kwanini bado wana nguvu kubwa nchi humo hata mara baada ya kumalizika kwa ubaguzi wa rangi.

Rais Mugabe alaumu namna wazazi walivyowalea watoto wao na kuruhusu wazungu kuendelea kuonekana wana nguvu nchini Afrika Kusini.
Rais Mugabe alaumu namna wazazi walivyowalea watoto wao na kuruhusu wazungu kuendelea kuonekana wana nguvu nchini Afrika Kusini. Jekesai NJIKIZANA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Mugabe ametoa kauli hii ikiwa zimepita siku chache tu toka mke wake apewe kinga ya kidiplomasia na serikali ya Afrika Kusini baada ya kudaiwa kumjeruhi msichana mmoja mwanamitindo aliyemkuta chumbani kwa watoto wake wa kiume.

Rais Mugabe badala yake amelaumu namna wazazi walivyowalea watoto wao na kuruhusu wazungu kuendelea kuonekana wana nguvu.

Mwanzoni mwa mwezi Agosti shirika la wanaharakati nchini Afrika Kusini, Afriforum, lilitangaza nia yake ya kuwasilisha maombi yake mbele ya mahakama ya kutaka mkewe rais wa Zimbabwe Robert Mugabe aondolewe kinga ya kidiplomasia iliyotolewa na serikali ya Afrika Kusini.

Grace Mugabe anashtumiwa kumshambulia Gabriella Engels mjini Johannesburg, nchini Afrika Kusini.

"Tutaomba mahakama kusema kwamba uamuzi wa wa kumpa mkewe rais `mugabe kinga ya kidiplomasia ni kinyume cha sheria kwa sababu, kulingana na sheria yetu, kinga ya kidiplomasia haiwezi kutumika katika kesi kubwa ya uhalifu na unyanyasaji" Kallie Kriel, kiongozi wa Afriforum aliliambia shirika la habari la AFP.

Grace Mugabe alirejea nyumbani kutoka Afrika kusini licha ya kukabiliwa na mashtaka ya kushambulia mwanamitindo Gabriella Engels katika hoteli moja Johannesburg.

Inaeleweka kwamba Grace Mugabe alisafiri pamoja na mumewe kutoka Afrika Kusini.

Wawili hao walikuwa wanahudhuria mkutano wa kikanda Afrika kusini.

Mawakili wa Gabriella Engels mwanamke ambaye analaumu Bi Mugabe kwa kumgonga, wanasema kuwa mteja wao alipewa pesa kuachana na kesi hiyo lakini akakataa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.