Pata taarifa kuu
ANGOLA-UCHAGUZI

Chama tawala Angola chashinda uchaguzi, upinzani wapinga

Chama tawala nchini Angola MPLA kimeibuka msindi wa Uchaguzi Mkuu nchini Angola. Chama hiki ambacho kinatawala kwa miongo minne sasakimepata zaidi ya 64% ya kura.

Wafuasi wa Joao Lourenço, wakikusanyika kwa mkutano wa mgombea wa MPLA, Agosti 17, 2017, kabla ya uchaguzi mkuu Angola.
Wafuasi wa Joao Lourenço, wakikusanyika kwa mkutano wa mgombea wa MPLA, Agosti 17, 2017, kabla ya uchaguzi mkuu Angola. REUTERS/Stephen Eisenhammer
Matangazo ya kibiashara

Mgombea wa chama cah MPLA, Joao Lourenço, atamrithi rais Jose Eduardo dos Santos, ambaye aliamua kujiuzulu baada ya miaka 38 ya kuingoza Angola. Matokeo haya yamefutiliwa mbali na na vyama vikuu viwili vya upinzani.

Chama cha MPLA madarakani kwa miongo minne nchini Angola kimeshinda Uchaguzi Mkuu kwa 64.57% ya kura, kwa mujibu wa takwimu za awali kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kikiongoza mbele chama cha Unita ambacho kimepata 24.04%, Casa-Ce (8.56%) , PRS (1.37%), FNLA (0.95%) na APN (0.52%).

Baada ya kutangazwa kwa matokeo na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, wakala wa chama cha Unita alisimama kupinga matokeo yote kwa jumla mbele ya waandishi wa habari. Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, chama cha Unita kilichukua nafasi ya pili na kimepata 24.04% ya kura. Kwa upande wa chama cha upinzani cha kihistoria kimesema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeegemea kwa chama tawala cha MPLA. Chama hiki kimeahidi kura zake lakini tayari kimetangaza kuwa kimeshinda katika jimbo la Luanda, tofauti na matokeoyaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CNE) ambayo imekipa ushindi chama cha MPLA.

Kulingana na matokeo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, chama tawala kimeshinda katika mikoa yote, ingawa kura zake ziko chini ya zile kilizopata mwaka 2012 katika maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na zile kilizopata katika mji mkuu Luanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.