Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-AFRIKA KUSINI

Serikali ya Afrika Kusini yashtakiwa kuondoa kinga ya kidiplomasia kwa Bi. Mugabe

Mwanamke mwenye umri wa miaka 20 aliyedai kupigwa na kujeruhiwa na Bi. Grace Mugabe, mke wa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, amekwenda Mahakamani kulalamikia hatua ya serikali kumpa kinga ya kidiplomasia na kumtofungulia mashtaka Bi. Mugabe.

Grace Mugabe, mke wa rais wa Zimbbawe Robert Mugabe
Grace Mugabe, mke wa rais wa Zimbbawe Robert Mugabe REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Afrika Kusini badala yake ilijitetea na kusema ilichukua hatua hiyo kwa sababu Bi.Mugabe ana kinga ya kidiplomasia na hivyo asingeweza kupelekwa Mahakamani.

Mwanamke huyo Gabriella Engels ameendelea kusisitiza kuwa alivamiwa na kifaa cha umeme jijini Johannesburg katika hoteli ambayo Bi.Mugabe na wanawe wawili wa kiume walikuwa wanaishi.

Engels anaitaka Mahakama kubadilisha kinga ya kidiplomasia aliyopewa Bi.Mugabe na kumsadia kurudi nyumbani na kuweka wazi kuwa haizuii kushtakiwa kwake Mahakamani.

Kesi hiyo imeratibiwa kusikilizwa tarehe 19 mwezi Septemba.

Wanaharakati na wanasiasa wa upinzani pia wamelaani hatua ya serikali ya Afrika Kusini kumruhusu Bi.Mugabe kuondoka nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.