Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-UN

Sudani Kusini yavutana na UN kuhusu nani alinde uwanja wa ndege wa Juba

Serikali ya Juba na walinda amani wa umoja wa Mataifa wameendelea kuvutana kuhusu nani mwenye mamlaka ya kuulinda uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sudan Kusini.

Walinda amani wa umoja wa Mataifa walioko nchini Sudan Kusini. Picha ya Maktaba 19 July 2016
Walinda amani wa umoja wa Mataifa walioko nchini Sudan Kusini. Picha ya Maktaba 19 July 2016 UN Photo/Eric Kanalstein
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wa kulinda amani elfu 4 waliowasili hivi majuzi mjini Juba, Sudan Kusini wamekuwa wakilinda uwanja wa ndege wa kimataifa wa Juba hatua ambayo haijaungwa mkono hata chembe na Serikali.

Hapo jana msemaji wa rais Salva Kiir, Ateny Wek Ateny alisema Serikali yao haitakubali kuona inapokwa mamlaka ya kulinda uwanja wa ndege wa Juba, kwa kuwa suala hilo ni la mamlaka ya ndani na sio vikosi vya Kigeni.

Utawala wa Juba unasema vikosi hivyo havikupewa mamlaka ya kulinda uwanja wa ndege wa Juba badala yake vilipewa mamlaka ya kulinda raia kwenye mji huo na maeneo mengine ya nchi.

Kiongozi wa wanajeshi wa umoja wa Mataifa wanaolinda uwanja wa ndege wa Juba, David Sherer, amesema kuwa uwepo wao hauna maana yoyote mbaya kwa utawala wa Juba.

"Tuna ndege nyingi ambazo zinaruka na kutua hapa kwenye uwanja wa ndege wa Juba kupeleka misaada kwenye maeneo tofauti ya nchi lakini pia wanajeshi wetu wanasafirishwa kwa ndege hizo hizo". amesema David.

Sherer ameongeza kuwa "wanajeshi wetu wanajukumu la kufanya kila wawezalo kulinda raia wasishambuliwe na vikosi vya Serikali ama magenge mengine yenye silaha."

Hata hivyo uamuzi huu haujaifurahisha Serikali ya Sudan Kusini, ambapo kaimu msemaji rasmi wa jeshi la nchi hiyo, Lul Ruai Koang ambaye amesema wao kama wanajeshi wanaolinda uwanja huo ni lazima wajue walinda amani hao wanaleta nini nchini humo.

Wadadisi wa mambo wanaona kuwa mvutano huu huenda ukachelewesha pia kuwasili kwa wanajeshi wote elfu 4 wanaotakiwa kuwa wamewasili nchini humo kulinda amani chini ya azimio la baraza la usalama la umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.