Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-MUGABE-USALAMA

Polisi ya Afrika Kusini yapewa agizo la kumzuia Bi Mugabe

Waziri wa polisi wa Afrika Kusini ametoa agizo kwa maafisa wa usalama wa Mipakani kuwa makini kwa kuhakikisha kuwa mkewe rais Mugabe asifurukuti kuvuka mipaka ya taifa hilo kwenda nchi jirani.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (kushoto) na mkewe Grace Mugabe (kulia).
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (kushoto) na mkewe Grace Mugabe (kulia). ( Photo : Alexander Joe /AFP )
Matangazo ya kibiashara

Grace Mugabe anatuhumiwa kumpiga na kumjeruhi Gabriela Engels , mwanamke mwenye umri wa miaka 20 katika kichwa chake katika chumba cha hoteli karibu na mji wa Johannesburg .

Bi Mugabe hajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.

“Sisi polisi wa Afrika Kusini tayari tumeweka notisi katika mipaka yetu yote ili kumzuia bi Mugabe kuondoka nchini siku ya Jumatano” , Waziri wa polisi Fikile Mbalula alisema.

Kumekuwa na taarifa kuwa familia ya mwanamitindo, Gabriella Engels iliahidiwa kupewa kitita cha fedha ili iachane na kesi hiyo, lakini mawakili wake wamekataa wakisisitiza azma yao ya kumfikisha mahakamani.

Tayari rais Mugabe amesafiri kwenda nchini Afrika Kusini kujaribu kumaliza sintofahamu inayomkabili mke wake, huku wanaharakati wakipinga kuhusu kiongozi huyo kulindwa kwa kutumia kinga ya kidiplomasia.

Mkewe rais Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 52, kwa sasa hajulikani alipo. Baadhi ya maafisa wa usalama nchini Afrika Kusini wanaamini kwamba bado yupo Afrika Kusini.

Polisi wanasema Grace Mugabe alipaswa kuripoti siku ya mbele yao siku ya Jumanne lakini hakufanya hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.