Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-AFRIKA KUSINI

Shinikizo zatolewa kwa mke wa rais Mugabe kufunguliwa mashtaka

Afrika Kusini inashinikizwa kuhakikisha kuwa mke wa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe anafunguliwa mashtaka baada ya kutuhumiwa kumpiga na kumjeruhi mwanamke mmoja nchini humo wiki iliyopita kwa kutumia kifaa cha umeme.

Rais Robert Mugabe, mkewe anatuhumiwa kumpiga mwanamke nchini Afrika Kusini na kumjeruhi
Rais Robert Mugabe, mkewe anatuhumiwa kumpiga mwanamke nchini Afrika Kusini na kumjeruhi SEBASTIEN RIEUSSEC / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya Bi. Grace Mugabe kurejea nyumbani siku ya Jumatano bila ya kufikishwa Mahakamani, licha ya kutarajiwa kuwa angefika Mahakamani.

Ikiwa itakuwa hivyo, hali hii itazua hasira kubwa baada ya Afrika Kusini mwaka 2015 kushindwa kumkamata rais wa Sudan Omar Al Bashir anayetakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya ICC.

Mahakama nchini humo iliamua kuwa, serikali ilikosea kwa kutomkamata rais Bashir.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Afrika Kusini, yameendelea kushinikiza kufunguliwa mashtaka kwa Bi. Mugabe ambaye kurejea kwake nyumbani kumeshangaza wengi.

Wanaharakati wanataka mke wa Mugabe kufika Mahakamani, kukubali kosa na kutozwa faini .

Hali hii imezua wasiwasi wa kidiplomasia kati ya nchi hizo jirani, huku rais Jacob Zuma akitarajiwa kukutana na mwezake Robert Mugabe kujadili suala hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.