Pata taarifa kuu
ZAMBIA-UPINZANI

Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema aachiliwa huru

Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema ameachiliwa huru na mashtaka ya uhaini kuondolewa.

Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema baada ya kuachiliwa huru Agosti 16 2017 jijini Lusaka
Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema baada ya kuachiliwa huru Agosti 16 2017 jijini Lusaka https://twitter.com/UPNDZM
Matangazo ya kibiashara

Chama chake cha UPND kimesema kuwa kiongozi wao na watu wengine watano, wameachiliwa huru siku moja baada ya kesi yake kuanza katika Mahakama Kuu jijini Lusaka.

Hichilema amekuwa akizuiliwa tangu mwezi Aprili mwaka huu baada ya kukamatwa na kushtakiwa kwa kuzuia msafara wa rais Edgar Lungu.

Rais Lungu, alimshinda Hichilema mwaka uliopita katika Uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali, lakini Hichilema amekataa kumtambua Lungu kama rais na kusema kura zake ziliibiwa.

Hichilema alikuwa amekanusha madai hayo siku ya Jumatatu baada ya kesi yake kuanza na kupangwa kurejelewa siku ya Jumatano.

Upinzani umekuwa ukisema kiongozi wao amekuwa akinyanyaswa na kesi hiyo ilikuwa ya kisiasa.

Hata hivyo, serikali kupitia rais Edgar Lungu mwenyewe amekuwa akisema kuwa binafasi hajawahi kuagiza kukamatwa kwa mpinzani wake licha ya kutangaza hali ya hatari nchini humo.

Hadi kuachiliwa kwake, Hichilema amekuwa akiituhumu serikali kutaka kumdhuru kwa kumzuia katika mazingira magumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.