Pata taarifa kuu
SIERRA LEONE-USALAMA

Idadi ya vifo yaongezeka Sierra Leone

Wakati ambapo zoezi la kutafuta miili mingine likiendelea katika wilaya yenye milima ya Regent katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown, inaripotiwa kuwa idadi ya waathirika wa maporomoko ya udongo imeongezeka na kufika mia nne.

Katika wilaya ya Regent, sehemu moja ya wilaya hiyo iliahtirika kwa maji, siku ya Jumatatu, Agosti 14. zaidi ya watu 300 walipoteza maisha.
Katika wilaya ya Regent, sehemu moja ya wilaya hiyo iliahtirika kwa maji, siku ya Jumatatu, Agosti 14. zaidi ya watu 300 walipoteza maisha. REUTERS/Ernest Henry
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa usalama wamesema kwa zaidi ya miili mia moja imetolewa chini vifusi siku ya Jumanne na maiti zinaendelea kupatikana kutokana na zoezi gumu la uokozi linaloendelea.

Rais wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma, ameomba msaada wa dharura kwa nchi yake ili usaidie nchi hiyo kukabiliana na “uharibifu wa hali ya juu”.

Mazishi ya pamoja yamepangwa ili kupunguza msongamano wa maiti katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Mpaka siku ya Jumatatu miili zaidi ya mia tatu ilikua imepatikana, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Sierra Leone.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.