Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Polisi ya DRC yalihusisha kundi la Bundu dia Mayala kwa machafuko

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, watu kumi na wawili waliuawa katika mji wa Kinshasa siku ya Jumatatu, polisi imesema. Polisi imewahusisha wafuasi wa kundi la Bundu dia Kongo kwa machafuko hayo.

Mji mkuu wa DRC, Kinshasa, ambapo mauaji ya watu kumi na wawili yalitokea.
Mji mkuu wa DRC, Kinshasa, ambapo mauaji ya watu kumi na wawili yalitokea. Wikimedia/Moyogo
Matangazo ya kibiashara

Polisi ya DRC imehakikisha kwamba hali ya utulivu imerejea katika mji wa Kinshasa, na miji mingine kama vile Boma na Matadi, miji miwili ya Congo ya Kati ambapo maandamano pia yalishuhudiwa mapema asubuhi.

Kwenye saa 9, waandamanaji waliobeba mabango yenye rangi nyekundu waliandamana karibu na gereza kuu la mji wa Kinshasa. Mashahidi kadhaa wanasema walisikia milio ya risasi, huku polisi ikitumia mabomu ya machozi. Maandamano pia yalishuhudiwa katika mkoa wa Congo ya Kati, hasa katika miji ya Boma na Matadi.

Kwa mujibu wa takwimu za serikali, watu 12 waliuawa katika mji wa Kinshasa wakati vurugu hizo. "Wauaji" kwa mujibu wa polisi, lakini vyanzo vingine katika mji mkuu wa DRC wamesema miili zaidi ya 20 ilioneka katika mitaa ya mji wa Kinshasa. Watu wawili waliuawa katika mji wa Matadi, pia walielezwa na polisi kuwa ni wauaji na polisi watatu walijeruhiwa vibaya. Katika mji wa Kinshasa, Naibu mkuu wa polisi katika mji huo alipigwa mawe na hali yake ya afya iko mbaya, na Afisa Mkuu wa polisi katika mji wa Kinshasa aliuawa, kwa mujibu wa vyanzo vya usalama mjini Kinshasa.

Polisi imewahusisha wafuasi wa kundi la Bundu dia Mayala kwa machafuko hayo. Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, watu hawa walikuwa walijihami kwa silaha za kivita na visu. "Wanataka kuondoka kwa viongozi walio madarakani," amesema msemaji wa polisi Kanali Mwanamputu Empung. "Huo sio utaratibu. Inabidi kufanyike uchaguzi, huo ndio utaratibu mzuri, "ameongeza kanali Empung.

“Vikosi vya usalama kwa bahati nzuri, kutokana na taaluma yao vimeweza kurejesha utulivu katika miji hii, “ amesema msemaji wa polisi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kundi la Bundu dia Kongo lililoundwa mwaka 1986 na Muanda Nsemi, limeendelea kukumbwa na ukandamizaji unaotekelezwa na baadhi ya polisi kwa amri ya baadhi ya maafisa wa usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.