Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ZUMA-MAANDAMANO

Mvutano waongezeka kuhusu rais Jacob Zuma Afrika Kusini

Nchini Afrika ya Kusini, mvutano unaendelea kuongezeka wakati ambapo wabunge wanatarajia kutathmini siku ya Jumanne Agosti 8 kura ya kutokua na imani dhidi ya rais Jacob Zuma. Uamuzi uliopitishwa na upinzani mnamo mwezi Machi.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, hapa katika mkutano na waandishi wa habari mjini Harare, Zimbabwe, Novemba 3, 2016.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, hapa katika mkutano na waandishi wa habari mjini Harare, Zimbabwe, Novemba 3, 2016. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Upinzani uliomba kura hii ipigwe iwe ya siri katika matumaini ya kujiunga na kundi la wabunge kutoka chama tawala cha ANC ambao wanampinga Jacob Zauma.

Kesi hii ilifikishwa kwenye Mahakama ya Katiba, ambayo iliamua kuwa kura hii iwe ya siri, licha ya uamuzi wa mwisho unatakiwa kutoka kwa Spoika wa Bunge, Baleka Mbete. Ikiwa imesalia siku moja tu kabla ya kura hiyo, Spika wa Bunge bado hajatoa uamuzi wake wakati ambapo maandamano makubwa yanatazamiwa kufanyika leo Jumatatu na kesho Jumanne nchini kote.

Ukimya wa Spika wa Bunge unasababisha msukosuko nchini Afrika Kusini. Baadhi wanamshtumu Baleka Mbete wamba anataka kupoteza mudaili kusubiri dakika ya mwisho atangaze kwamba kura ya kutokua na imani dhidi ya rais Maduro haitokua ya siri. Njia mojawepo, pengine, kwa Spika wa Bunge kukwepa ukosoaji wa upinzani na kuepuka hatua ya mwisho ya upinzani kwenda mahakamani.

Wakati huo huo, kila mmoja amechukua msimamo wake. Kiongozi wa kundi la wabunge kutoka chama cha ANC ameelezea kwamba ni jambo la "kutofikiria" kuwa wabunge wa chama hicho watapiga kura ya kutokua na imani dhidi ya rais Zuma. "Hali hii itasababisha mgogoro isiyokuwa wa kawaida," ameonya. Chama cha ANC tayari kimechukuliwa hatua za kinidhamu dhidi ya mbunge ambaye ataunga mkono hadharani kura ya siri.

Chma cha cha Kikomunisti nchini Afrika Kusini ambacho ni mshirika wa kihistoria wa chama cvha ANCkimewataka wabunge wake 17 kukataa kura ya kutokuwa na imani dhidi ya rais Zuma ili kutoiadhibu serikali kwa ujumla. Lakini mazungumzo yanapaswa kuanza kuhusu mustakabali wa Jacob Zuma.

Kwa upande wa chama cha wafanyakazi cha Cosatu,kimetoa wito kwa wajumbe wake kujiunga katika maandamano ya siku ya Jumatatu na Jumanne mjini Cape Town na Johannesburg ili kumuomba rais Zuma ajiuzulu.

Chama cha ANC kina wabunge 249 kwa jumla ya wabunge 400 wa Bunge la taifa nchini Afrika Kusini. Ikiwa Wabunge 50 kutoka chama cha ANC watakubali kujiunga na upinzani, hakuna shaka kuwa rais Zuma atakua amefikia hatua ya kuondoka mamlakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.