Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Italia kukabiliana na wahamiaji wanaotokea Libya

media Wanaharakati wa haki za binadamu wanahofia kuwa hatua ya Itali ya kuwazuai wa hamiaji itawafanya wahamiaji zaidi kukiuka sheria za uhamiaji ikiwa watarejeshwa Libya. Reuters/Stefano Rellandini

Bunge la Italia limepitisha mpango wa kutuma meli za kivita katika bahari ya Libya kuwazuia wahamiaji kutoka Libya kuvuka bahari ya Meditarenia. Itala haitaki wahamiaji na wakimbizi zaidi wanaowasili nchini humo.

Kura ya hivi karibuni ya bunge iliashiria mwanzo wa mafanikio ya azma ya taifa hilo kuwarudisha nyuma wahamiaji na wakimbizi katikati mwa bahari ya Mediterranean.

Wanaharakati wa haki za binadamu wanahofia kuwa hatua hii ya Italia itawafanya wahamiaji zaidi kukiuka sheria za uhamiaji ikiwa watarejeshwa Libya.

Wahamiaji wanaohifadhiwa wanaishi mazingira duni, huku ikiaminika kuwa wamekua wakifanyiwa vitendo udhalili kama kupigwa na hata kubakwa.

Italia ni nchi inayopokea wahamiaji wengi wanaosafiri kutoka Libya, nchi ambayo inaaminika kuwa kitovu cha wahamiaji wengi kutoka kusini mwa jangwa la Sahara kuingia Ulaya.

Hivi karibuni wizara ya ulinzi ya Itali ilituma meli mbili ndani ya eneo la maji la Libya kusaidia walinzi wa mwambao wa Libya kukabiliana na wahamiaji wanaoelekea Ulaya kupitia Itali.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana