Pata taarifa kuu
SOMALIA

Uganda yathibitisha kuuawa kwa wanajeshi wake nchini Somalia

Jeshi la Uganda limethibitisha kuuawa kwa wanajeshi wake 12, waliovamiwa na magaidi wa Al Shabab nchini Somalia mwishoni mwa wiki iliyopita.

Shambulizi la kigaidi mjini Mogadishu nchini Somalia
Shambulizi la kigaidi mjini Mogadishu nchini Somalia AFP photo
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Jeshi hilo Brigedia Richard Karemire amesema kikosi hicho kinachohudumu katika jeshi la Umoja wa Afrika AMISOM, walivamiwa Kusini mwa nchi hiyo.

Aidha, ameongeza kuwa wanajeshi wengine saba wamejeruhiwa na wanapata matibabu katika Hospitali jijini Mogadishu.

Uchunguzi umeanza kubaini mazingira ya kushambuliwa kwa wanajeshi hao wa UPDF katika mazingira ya kushtukiza na kutatanisha wakati wakipiga doria katika eneo la Gorowen.

Hata hivyo, Al Shabab inasema iliwauwa wanajeshi 39 wakiwemo Makanda wa jeshi hilo madai ambayo AMISOM imekanusa.

Jeshi la Umoja wa Afrika lina wanajeshi 22,000 nchini Somalia wanaoungwa mkono Kimataifa kuwashinda wanamgambo wa Al Shabab.

Uganda inaendelea kuwa na wanajeshi wengi nchini Somalia wapatao elfu Sita.

Mataifa mengine yaliyo na vikosi nchini humo ni oamomija na Burundi, Ethiopia, Kenya na Djibouti.

Nigeria na Ghana wametuma maafisa wa Polisi.

Lengo la vikosi hivi ni kuisaidia Somalia kupambana na kuwashinda magaidi wa Al Shabab na kuiunga mkono serikali ya Mogadishu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.