Pata taarifa kuu
CAR-MINUSCA-USALAMA

MINUSCA yatuma askari wengi katika mji wa Bangassou

Askari tisa wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) wameuawa nchini humo tangu mwanzoni mwa mwaka huu, ikiwa ni pamoja na watatu tangu Jumapili katika mji wa Bangassou.

Msafara wa MINUSCA  njiani kuelekea katika miji ya Bambari na Ippy (picha ya zamani).
Msafara wa MINUSCA njiani kuelekea katika miji ya Bambari na Ippy (picha ya zamani). © RFI/Pierre Pinto
Matangazo ya kibiashara

Mji wa Bangassou unakabiliwa na hali ya wasiwasi tangu kundi wanamgambo wenye silaha, kwa miezi kadhaa iliyopita, liliamua kushikilia baadhi ya maeneo na kushambulia watu kutoka jamii ya Waislamu. Kikosi cha askari wa Umoja wa Mataifa (MINUSCA) kimechukua uamuzi wa kujibu mashambulizi hayo.

Kikosi hiki cha askari maalum kutoka Bangladeshi kinatazamiwa kuwasili katika mji wa Bangassou hadi mwishoni mwa wiki hii, MiNUSCA imebaini. Askari hawa ambao, tayari waliendesha shughuli kama hii katika mji wa Bambari na katika mji wa Ippy mwishoni mwa majira ya baridi yaliyopta, wakati wa ghasia kati ya makundi mawili hasimu ya samani ya Seleka, yatasaidiwa na vikosi vya kulinda amani kutoka Gabon pamoja na kitengo cha polisi kutoka Rwanda .

Kazi yao ni kurejesha amani na kuwalinda wakazi wa mji huu unaopatikana kilomita zaidi ya 700 kutoka mji wa Bangui na ambao unakumbwa na machafuko tangu mwezi Mei.

Wakati ambapo kikosi cha askari kutoka Morocco kikiendelea kusumbuliwa na makundi ya wanamgambo yanayodhibiti mji huo Bangassou, watu kutoka jamii ya Waislamu waliokimbilia karibu na kanisa kuu la mjini humo, ambao wanakabiliwa na ukosefu wa chakula wamezingirwa na wanamgambo haowao. Kwa ghadhabu, idadi ndogo yawatu hao kutoka jamii ya Waislam walipora katika kanisa hilo na kuharibu mali ya kanisa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kwa upande wa Padre Florentine Nzingazo, ambaye iko eneo hilo, amesema vikosi maalum vya MINUSCA vinahitajika kufika haraka sehemu hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.