Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI

Upinzani waja na mkakati kumshinikiza raisi Kabila kuachia madaraka

Upinzani nchini DRC umebainisha mipango yake kushinikiza kuondoka madarakani kwa raisi Joseph Kabila kwa kutumia migomo na kutokuwa na utii wa kiraia.

Upinzani kupitia chama cha UDPS chajiandaa kushinikiza raisi Kabila kuondoka madarakani
Upinzani kupitia chama cha UDPS chajiandaa kushinikiza raisi Kabila kuondoka madarakani Junior KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo linakuja baada ya siku mbili za mazungumzo ya upinzani jijini Kinshasa kufuatia wasiwasi kuwa raisi Kabila anayetawala taifa hilo tangu mwaka 2001 huenda akasalia madarakani zaidi kinyume cha katiba.

Uchaguzi ulitakiwa kufanyika mwaka huu nchini Drc Chini ya mkataba uliokusudia kuepusha vurugu za kisiasa nchini humo baada ya raisi Kabila kushindwa kuondoka madarakani mara muda wake ulipotamatika December 2016.

Chini ya mkakati mpya upinzani umepanga kufanya mgomo wa kitaifa kuanzia August 8 kama ishara ya kuonya kwa mujibu wa Francois Muamba,wa upinzani.

Mnamoz August 20 upinzani umepanga kufanya maandamano mfululizo katika jiji kuu la kinshasa na majimbo 25.

Ikiwa rasi Kabila hatatangaza tarehe ya uchaguzi hadi kufikia mwishoni mwa Septemba hatatambulika tena kama raisi wa jamuhuri ifikapo Octobaer 1 alieleza Muamba,akiwa katika ofisi za makao makuu ya chama cha upinzani Union for Democracy and Social Progress (UDPS) mjini Kinshasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.