Pata taarifa kuu
MOROCCO-USALAMA

Polisi zaidi ya sabini wajeruhiwa katika makabiliano na waandamanaji Morocco

Makabiliano yaliyotokea siku ya Alhamisi mchana katika mji wa al Hoceima kaskazini mwa Morocco, kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji yalisababisha watu zaidi ya themanini kujeruhiwa kutoka pande zote mbili, kwa mujibu wa chanzo cha polisi.

Waandamanaji wakirushia mawe vikosi vya usalama, Julai 20, 2017 katika mji wa al Hoceima katika eneo Rif, Morocco.
Waandamanaji wakirushia mawe vikosi vya usalama, Julai 20, 2017 katika mji wa al Hoceima katika eneo Rif, Morocco. REUTERS/Youssef Boudlal
Matangazo ya kibiashara

"Polisi sabini na wawili walijeruhiwa baada ya kurushiwa mawe (...) upande wa waandamanaji walijeruhiwa watu kumi na moja baada ya polisi kutumia mabomu ya machozi," manispa ya jiji la al Hoceima likinukuliwa na shirik ala habari la MAP, limearifu siku ya Alhamisi.

Mji huu na maeneo jirani yalishuhudia siku ya Alhamisi makabiliano kati ya waandamanaji na polisi, ambao walitumia mabomu ya machozi na kutumia nguvu zaidi kuzuia maandamano makubwa yaliokua yamepangwa kufanyika.

"Majeruhi wote wameruhusiwa kutoka hospitali, ispoku tu wawili ambao hali yao ni mbaya", kwa mujibu wa manispa ya jiji la al Hoceima, ikibaini kwamba magari mawili ya olisi yaliharibiwa viabaya baada ya kuchomwa moto na baadhi ya waandamanaji katika mji wa Ajdir "karibu na Al Hoceima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.