Pata taarifa kuu
DRC-UN-MAUAJI

Mauaji ya wataalamu wa UN nchini DRC: mashahidi muhimu wakosekana katika kesi

Kesi ya washtumiwa wa mauaji ya wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa ilisikilizwa tena siku ya Jumatatu Julai 17. Mashahidi kadhaa muhimu waliotarajiwa kufika kusikilizwa katika mahakama ya kijeshi ya Kananga hawakufika.

Mji wa Kananga, mji mkuu wa Kasai ya Kati, ambao inasikilizwa kesi ya washtumiwa wa mauaji ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa Michael Sharp na Zaida Catalan.
Mji wa Kananga, mji mkuu wa Kasai ya Kati, ambao inasikilizwa kesi ya washtumiwa wa mauaji ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa Michael Sharp na Zaida Catalan. wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwao, afisa iliekua akisimamia operesheni katika eneo ambapo wataalam walikutwa waliuawa. Meja Mbuara Issa alihamishiwa Tshikapa. Pia hakuna taarifa kuhusu kiongozi alietajwa na washtumiwa wakuu, aliyekuwa kiongozi wa wanamgambo wanaodaiwa kushirikiana na na jeshi la DRC (FARDC).

Jean Bosco Mukanda ni shahidi mkuu kwa upande wa jeshi la DR Congo, Umoja wa Mataifa, masirika yasio ya kiserikali na waandishi wa habari. Alikua mtu wa kwanza kurusha hewani habari za mauaji ya wataalam hao Michael Sharp na Zaida Catalan na alishtumu makundi ya wanamgambo wa eneo hilo kuwa ndio walihusika na mauaji ya wataalam hao.

Jean Bosco Mukanda alisema kuwa makundi ya wanamgambo ya Moyo-Musuila na Mulumba-Muteba yalihusika na mauaji ya wataalam wa Umoja wa Mataifa.

Taarifa za Bw Mukanda zinakwenda sambamba na zile lizorushwa na radio ya Mbunge Clément Kanku, kiongozi wa zamani wa wanamgambo aliyebadi sura na kuwa mpashaji habari katika jeshi la DR Congo alisem akuwa laiona tukio zima. Jean Bosco Mukanda ni mmoja wa watu waliosaidia kugunduliwa kwa miili ya wataalam hao wawili.

Bw Mukanda ambaye alisema alitishiwa kwa miezi kadhaa na viongozi wa wanamgambo kutokana na ukaribu wake na jeshi anaonekana kuingizwa kila mahali.

Haijajulikana iwapo Jean Bosco Mukanda atatoa ushahidi wake katika kesi inayosikilizwa katika mahakam ya kijeshi ya Kananga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.