Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Wanajeshi 34 wa Cameroon hawajulikani waliko baada ya meli yao kuzama

media Ramani ya eneo ambalo meli ya kijeshi ya Cameroon ilikozama www.rfi.fr

Wanajeshi 34 wa Cameroon bado hawajapatikana, siku moja baada ya meli yao kuzama katika Pwani ya nchi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Ripoti zinasema kuwa, meli hiyo ilikuwa na abiria 37 ikielekea katika mji wa Bakassi.

Waziri wa Ulinzi Joseph Beti Assomo amesema wanajeshi watatu ndio waliokolewa wakiwa hai baada ya kuzama kwa meli hiyo.

“Wanajeshi 34 bado hawajukani waliko lakini watatu wameokolewa,” amesema Waziri Assomo.

Meli hiyo ilikuwa imewabeba wanajeshi wa nchi hiyo wanaoaminiwa kupambana na kundi la Boko Haram kutoka nchini Nigeria Kaskazini mwa nchi hiyo.

Wizara ya ulinzi nchini Cameroon imesema meli hiyo ilipoteza mawasiliano kuanzia mapema wakati ikitokea jijini Duala ikielekea Bakasi saa moja kabla ya kupoteza mawasiliano.

 

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana