Pata taarifa kuu
DRCONGO

Mauaji soko la Kinshasa yazua hofu

Naibu kamanda wa Polisi na msimamizi wa soko kuu jijini Kinshasa nchini DRC wameuawa jana Ijumaa baada ya ya kushambuliwa na watu wasiojulikana ambao pia waliwafungulia wafungwa , Polisi na Mashahidi wamesema.

Africanews
Matangazo ya kibiashara

Washambuliaji hao walishambulia ofisi ya msimamizi wa soko na kituo cha polisi sokoni na kuruhuru wafungwa waliokuwa wakishikiliwa gerezani kukimbia.

Muuzaji mmoja katika soko hilo aliyefamika kwa jina la Marie-Pauline Liyolo, ameiambia AFP kuwa "Kulikuwa na hofu (katika soko) kwa sababu ofisi ya msimamizi ilishambuliwa pamoja na seli za polisi ambapo wafungwa wameachiliwa huru.

Msemaji polisi Kanali Pierrot-Rombaut Mwanamputu ameiambia AFP kuwa kwa upande wa maafa wamempoteza msimamizi wa soko, na naibu kamanda wa polisi aitwaye Kamambunzu" wa kituo cha polisi cha katikati.

Aliongeza kuwa maofisa wa polisi sita wamejeruhiwa sana na kupelekwa hospitali,Pia vituo viwili vya polisi katika eneo la soko vimeteketezwa.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.